Friday, October 18, 2013

SWAHILI FASHION WEEK 2013 LAUNCHED.

Meneja Maboresho Swahili Fashion Week, Hamis K Omary akizungumzia uboreshwaji wa Swahili Fashion Week 2013.
Bw. Honest Arroyal,Mratibu wa Mitindo Swahili Fashion Week (Kulia) na Catherine Lumbanga, Mratibu wa Masoko Golden Tulip Hotel wakizungumzia ujio mpya wa Swahili Fashion Week 2013.
Happy Shame, (Kulia) Meneja Masoko wa EATV na Ea Radio akizungumzia mipango ya EATV na Radio juu ya Swahili Fashion Week mwaka huu.
Mratibu wa Masoko na Mauzo kutoka Hoteli ya Golden Tulip Bi. Catherine Lumbanga akizungumzia jinsi hoteli yao inafurahi kushirikiana Swahili Fashion Week kwa mwaka wa pili mfululizo.

Maonesho ya sita ya Swahili Fashion Week yatafanyika Golden Tulip Hotel kuanzia tarehe 5 mpaka 8 Desemba 2013, Dar Es Salaam, Tanzania.

Swahili Fashion week 2013 itakusanya wabunifu 40 kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kuonesha mitindo yao, yenye kwenda na wakati na kutegemewa kushika soko la Afrika Mashariki mwaka 2014.

“Swahili Fashion Week mwaka huu ina lengo la kuifikia jamii zaidi, na kukuza vipaji katika tasnia ya mitindo. Ni zaidi kuhusu kuthamini wabunifu wa kwetu na kuwatengezea jina,huku tukiwapeleka ngazi za juu zaidi kila mwaka” Akizungumza Bw. Washington Benbella, Meneja wa Swahili Fashion Week

Ukiwa ni mwaka wa 6 wa Swahili Fashion Week, Katika mashindano ya wabunifu wanaochipukia, Waandaaji wamependekeza dhima ya mwaka huu (theme) “Evolution” ambayo inawataka wabunifu chipukizi hao kubuni mavazi yanayoashiria mabadiliko, si lazima upya, ila yenye muonekano wa kitofauti na mzuri.

“Tunasisitiza jamii iunge mkono tasnia ya mitindo na kuvaa mavazi ya kikwetu, hasa kwa Tanzania. Vipaji vya nyumbani vinahitaji kukuzwa ili kufikia majina yanayotambulika duniani katika tasnia hii. Hisani huanza nyumbani, na ndio maana tunategemea kampuni pamoja na mashirika mbali mbali kusaidia tasnia ya mitindo” Hamis K Omary, Meneja Masoko Swahili Fashion Week.

Swahili Fashion week imedhaminiwa na EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel, Eventlites, Push Mobile, BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa), Ultimate Security, Global Outdoor Ltd na 361 Degrees.

Swahili Fashion Week is ni jukwaa la wabunifu wa mitindo na vito kutoka Nchi zinazozungumza Kiswahili na Bara la Afrika kwa ujumla Kuonyesha ubunifu wao, kutafuta masoko kwa ajili ya ubunifu na kujenga uhusiano na wateja pamoja na tasnia ya mitindo kimataifa

Hii ni kwa nia ya kusisitiza kukua kwa mitindo katika kanda ya
Afrika Mashariki na Kati na njia ya kipato ihusishayo tasnia ya ubunifu, huku ikitangaza wazo la “Made in Africa”

Swahili Fashion Week imeanzishwa na mbunifu mashuhuri Tanzania, Mustafa Hassanali mwaka 2008. Mpaka sasa ndio maonyesho makubwa ya mitindo katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

2013 Itakua ni maonyesho ya sita ya Swahili Fashion Week na Tuzo, ambayo yatafanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 5 – 8 Desemba 2013.
 
credit: LUKAZA BLOG
 
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment