Alichokisema Mtunisy kina point hasa kwa muigizaji anayejitambua hawezi kujichubua na sio muigizaji tu bali hata watu wa kawaida kujichubua si kuzuri kwa kuwa kuna madhara mengi kiafya ikiwemo kansa ya ngozi. kwa muigizaji inakuwa ngumu kumchezesha characters zenye asili ya kiafrika na kijijini kwani wengine wamejichubua mpaka ngozi kuwa na rangi zaidi ya tatu, nyeusi, nyekundu, njano, blue na kijani hujitokeza usoni kwa mtu aliyeathirika na matumizi ya mkorogo. Mara nyingi waigizaji wanaojichubua wakicheza scenes za vijijini hawavutii usoni kwani mashavu na uso huwa na viraka vyeusi au kahawia na kupoteza ule uasili wa kiafrika ,. Na ndiyo maana hata film makers wa wa Hollywood wanapotaka waigizaji kutoka afrika huwa wanataka wale wenye weusi wa asili au ngozi zao halisi kwa kuwa ndiyo waafrika halisi na sio wale wanaoukana uafrika kwa kujichubua. Vile vile kujichubua ni ishara ya kutokujiamini katika ngozi yako halisi kwa mujibu wa wataalaam wa saikolojia. BE PROUD AFRICAN!!!
Mtunisy
No comments:
Post a Comment