Pages

Monday, October 21, 2013

BADO NAMPENDA SANA HASHEEM THABIT KULIKO DIAMOND, SINA TATIZO NA WEMA SEPETU: JOKATE MWEGELO

Jokate
Jokate Mwegelo amabye ni actress, model, fashion designer, MC, Chanel O presenter na mjasiriamali amesema kuwa licha ya kuachana na Hasheem Thabit lakini bado anampenda kwakuwa ndiye mwanaume aliyeonyesha kumjali. Jokate alionekana kumpa alama za juu Hasheem katika mapenzi kuliko Diamond Platinumz na moja ya sababu ya kumwagana na Diamond ikiwa ni mwanamuziki huyo kujitangaza katika media kwa kila demu anayetoka nae kimapenzi kitu ambacho Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2 wa mwaka 2006 hakukipenda. Akizungumza na GPL Jokate alisema "kugombana ni sehemu ya mapenzi, ni kuonyesha kuwa mnapendana, ilitokea hivyo kwangu kwasababu Hasheem alikuwa na heshima tofauti na wanaume wengine, nahisi hakuna kama yeye, alinionesha alikuwa ananijali kwa kiasi gani"

Jokate alipoulizwa kati ya Diamond na Hasheem ambaye ni mchezaji wa basketball nchini Marekani nani akimrudia atakubali alijibu kwa kusema "hakuna lakini ukweli nilimpenda sana Hasheem" aliongeza kwa kusisitiza "yap...nilimpenda na ninampenda sana"

Jokate alisema kuwa uhusiano wake na Hsheem ulidumu kati ya miaka 2-3 wakati yeye na Diamond walidumu kwa miezi miwili pekee. Kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu kwasasa ambaye alikuwa mpenzi wa Diamond kabla ya kumwaga na kuwa na yeye Jokate alisema "simchukii Wema, sina tatizo naye, unajua lilipotokea lile tatizo la yeye kunikashifu niliona nikiendeleza malumbano haitakuwa busara"

                                                 Jokate na Hasheem
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

2 comments:

  1. mhh ! Jokate huvumi lakini nawe umo...basi sawa mamaa hasheem atakusoma

    ReplyDelete
  2. tatizo unalo na wema sababu ulimnyima amani kwa makusudi,ukijua kabisa diamond ni moyo wake na ulijua kama anatoka naye zaidi ya hayo alimvisha pete lakini wewe ukajitia kiziwi na kipofu kana kwamba huuoni uhusiano wao.wanaume siku zote ni watu wakujaribu tu ukikubali basi anakupitia ndicho alichofanya diamond nawe ukajitia umepata bilakujua mwenzio yuko kitamaa zaidi nawe ukafunua mapembe yako uliupate kick mjini pole

    ReplyDelete