Actress maarufu Swahiliwood Irene Paul amemsifia muigizaji mwenzake wa filamu Van Vicker ambaye pia ni muigizaji maarufu hasa Afrika ya magharibi akitokea Ghana kwa kusema kuwa ni mkali katika scenes za kimapenzi. Irene ambaye kwasasa ni mmoja wa waigizaji wa kike walio juu aliyasema hayo kufuatia kuigiza filamu mpya na Van Vicker na wawili hao kukutana katika scene ya kimapenzi kitandani na Vicker kuonyesha uwezo mkubwa na kujiamini sana mpaka kufikia Irene Paul kuingiwa na hofu.
Paul amesema pia kuwa amefurahi kuigiza pamoja na Van Vicker kwani wapo waigizaji wengine wa kike walikuwa na ndoto ya kuigiza nae pia "jamaa utadhani tunafahamiana, alinikabili kitandani kwa kiwango kikubwa sana, nilipata hofu kubwa mno. Van anajua kuigiza jamani, kwangu hii ni bahati ambayo namshukuru mungu kuipata, wengi waliililia" alisema Paul akizungumza na Globalpublishers.
Van Vicker alikuwa nchini Tanzania na kuondoka wiki iliyopita baada ya kukamilisha shooting yake na mastaa wa Swahiliwood kama vile Hashim Kambi, Wellu Sengo, Slim Omar, Sandra na Irene Paul.
Irene Paul na Van Vicker
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news.
No comments:
Post a Comment