Sunday, September 8, 2013

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA, MUIGIZAJI WA FILAMU LIBERTY MSUYA APEKULIWA AIRPORT.

Liberty aliyevaa vest nyekundu
Liberty Msuya ambaye ni mfanyabiashara maarufu na msanii nyota wa filamu Swahiliwood ambaye pia ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu katikati ya wiki hii alionja joto ya jiwe baada ya kuhenyeshwa masaa kadhaa kwa kupekuliwa alipokuwa anareja toka nchini Uingereza huku msanii mwenzake Manaiki Sanga akihangaika kumnusuru.


Habari zilizonaswa na Xdjz ambayo ilikuwepo kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kumpokea mzanii Azonto ambapo Libarty alisafiri ndege moja na Azonto wakitokea Uingereza ilishuhudia issue hiyo sehemu ya kutokea wageni wanaokuwa wanawasili.


Libert Msuya ambae ana uraia wa Ungereza licha ya kwamba ni mtanzania siku za hivi karibuni alikuwa nchini huko ambapo ndio familia yake ilipo na siku hiyo ya tukio alikuwa anarejea Tanzania huku akiwa na mabegi kibao na baada ya kufika AirPort ya Dar es salaam na mabegi hayo alifanyiwa uchunguzi mkubwa kiasi cha kusababisha askari wote kumzunguka.

Hata hivyo hali hiyo iliyodumu kwa dakika 40 ilimlazimu rafiki yake wa karibu Manaiki Sanga kuanza kuchanganyikiwa akizani labda huenda ni kweli rafiki yake huyo alikuwa na mzigo.


Aidha baada ya kuachiwa huru Liberty alitoka nje huku akipokelewa na Manaiki. Mwandishi alifanikiwa kuongea na Liberty ambaye alisema Ni utaratibu ambao upo kila nchi wa kusachiwa hivyo mimi sikuona tatizo pele na wala mimi sijihusishi na biashara yoyote haramu


  Nae msanii Manaiki Sanga” The Done”  alisema  kuwa biashara ya madawa sio rahisi kwa kuwa  inafanywa na watu wenye mioyo migumu huku wakiwa wamekula viapo kwamba lolote litakalotokea poa na sio kazi rahisi kama sanaa wanayoifanya wasanii.


 Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood new

No comments:

Post a Comment