Tuesday, September 17, 2013

MASANJA AFUNGUKA BAADA YA KUDAIWA KUNYANG'ANYWA PASSPORT NA SERIKALI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA.

Hivi karibuni kulienea habari kwenye mitandao ya kijamii, blogs na hata magazetini kuwa muigizaji maarufu nchini Masanja Mkandamizaji na mwanamuziki Diamond Platinumz wamenyang'anywa passport zao na serikali kufuatia kushukiwa kujihusisha na dawa za kulevya. Hata hivyo leo kupitia mtandao wa twitter Masanja ambaye siku hizi anajihusisha na mambo ya kiroho pia amekanusha habari hizo kwa kuandika "wengi wananiuliza kuhusu tuhuma za passport yangu kushikiliwa na serikali na kwamba mimi nachunguzwa kuhusu madawa ya kulevya, si kweli !"

Inadaiwa kuwa mastaa hao walishukiwa kufuatia utajiri wa haraka walioupata huku ghorofa la Masanja likiwa moja ya kushukiwa kwake kujihusisha na biashara hiyo haramu.


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment