Pages

Tuesday, September 24, 2013

KUWA MAKINI NA MATAPELI PAGE YA BATULI FACEBOOK IMEHAKIWA(HACKED) LEO.

Fan page ya Facebook ya muigizaji maarufu wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) imehakiwa(hacked) na watu wasiojulikana ambao wanaaminika kuwa ni matapeli wa mitandaoni wakijifanya kutoa mikopo isiyo na riba. Batuli ameiambia Swahiliworldplanet kuwa akaunti yake imehakiwa leo na anaomba watanzania wajue kuwa siyo yeye ila watu hao hawana nia nzuri kwake. Matapeli hao wameandika hivi
 "ONYO: Epuka matapeli wanaojiita Tanzania Loan, Jakaya Foundation na Zitto Kabwe Foundation wanaojinadi kuwa wanatoa mikopo. Hao ni matapeli Taasisi inayotoa mikopo nafuu isiyokua na riba ni taasisi moja tu! Inaitwa SAVING FOUNDATION ni taasisi ya serikali hii ndio inayotoa mikopo peke yake, kwa mtu yoyote anaetaka mkopo wa pesa namshauri ajiunge na SAVING FOUNDATION kwani mikopo yao haina riba, nafuu na rahisi"

Matapeli hao wamekuwa waki-hack akaunti na page nyingi za watu au vipindi maarufu na kuingia kisha kuandika na kupost wanavyotaka ili kuwaaminisha watu washawishike kirahisi kujiunga na taasisi hiyo ya kitapeli ambapo mtu hujiunga kwa ada na ukiingia mkenge kujiunga kwa matarajio ya kupata mkopo ndiyo imekula kwako maana pesa inaenda halafu hakuna cha mkopo wala nini. Diamond platinumz pia aliwahi kukiri akaunt yake kuhakiwa na watu hao na hivi karibuni walidaiwa ku-hack akaunt ya The Mboni Show na EATV.

Pia Zito kabwe alishaelezea mara nyingi kuwa hana foundation ya aina yoyote kama ilivyotajwa hapo juu hivyo watu wawe makini na matapeli, na hata mheshimiwa Rais kikwete hana foundation yoyote ya kutoa mikopo bila riba. Fan Page ya Batuli iliyohakiwa(hacked) ni hii hapa BATULI ACTRESS

                                                        Batuli
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

5 comments:

  1. Very sad pole batuli

    ReplyDelete
  2. JAMANI THANK YOU KWA TAARIFA VERY SORRY BATULI WANGU. SAMIRA

    ReplyDelete
  3. Pole BATULI FUNGUA FAN PAGE MPYA MADAM TUPO PAMOJA. GERE

    ReplyDelete
  4. Ushauri kwako;
    1.Sali sana 2.Toa sadaka usiku na mchana 3.Moyo wako uwe safi muda wote 4.Samehe wanaokukosea na Waombe msamaha unaowakosea 5.Chapakazi 6.Usibadilike kitabia 7.Anaekurekebisha anakupenda usimchukie 8.Magazeti ya udaku yasikukatishe tamaa hata waandike nini wewe songa mbele na washangaze walimwengu 9.Hakuna rafiki mzuri amini bongo movie ndio adui zako namba moja 10.Hili ndilo kubwa kuliko yote naomba nikuambie wewe ni mwanamke mrembo sana na kwa sasa huna mpinzani kwenye kazi kina lako linakua siku hadi siku na jina hilo linakuwa kwa heshma na hadhi kubwa wapo watakaopambana na wewe ili wakuporomoshe lakini ukizingatia niliyokuambia hakika hawataweza. BATULI NAKUTAKIA KILA LA KHERI KWENYE KAZI ZAKO NAKUBARIKI KAMA MWANANGU WS KUKUZAA NAJUA HUNIFAHAMU ILA NIHESABU KAMA MZAZI WAKO NAITWA MAMA KAHENA NAISHI MWANZA KARIBU NA HOTEL YA MWANZA HOTEL JINA LANGU NI MAARUFU ENEO HILO. SALAMU KWA WAZAZI WAKO NA WANAO

    ReplyDelete
  5. God is with you pretty Batuli usiumie sana muachie Mungu

    ReplyDelete