Pages

Thursday, September 5, 2013

DIAMOND NI KAMA ALIVYOKUWA KANUMBA: DULLY SYKES

Dully Sykes ambaye ni mwanamuziki maarufu wa Bongofleva amezipongeza juhudi za Diamond katika kujitangaza kimuziki kimataifa kwa kufanya kazi bora kufuatia video yake mpya ya My Number One kupongezwa na watu wengi. Video hiyo imefanyikia S.Afrika na kugharimu $30,000 takribani zaidi ya Tsh.milioni 45. Dully amesema kuwa marehemu Steven Kanumba alikuwa mtu wa kuthubutu kama Diamond ndiyo maana alifika mbali na kujulikana sana. Akizungumza na Bongo5 Dully alisema "Kanumba alikuwa ana uwezo wa hata kuchukua nauli yake ya kwenda sehemu kama Ghana kwenye tamasha la movie lakini ilimradi kujitengenezea status yake. Kwa hiyo Diamond ni mtu ambaye tayari ameshajitolea kwaajili ya kuutetea muziki wetu"

                                                             Diamond
  Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood new

No comments:

Post a Comment