Wema Sepetu anadaiwa kutotaka skendo siku hizi kwa madai kuwa zimekuwa zikimchafua sana huku baadhi ya mastaa wenzake wenye majina makubwa wakiwa juu bila skendo yoyote na kuendelea kufanya vizuri kwenye tasnia ya filamu. Chanzo kimoja kilicho karibu na Wema kikizungumza jana na Swahiliworldplanet kwa masharti ya kutotajwa jina lake kilisema kuwa Wema amekuwa akiumizwa sana na skendo zake hivyo siku hizi amekuwa akihakikisha hachafuki hovyo hasa kwenye magazeti ya udaku na mitandaoni. Chanzo hicho kiliongeza kwa kusema kuwa hata kimavazi Wema amebadilika siku hizi. "Wema hataki scandals now unajua hata yeye mwenyewe anajua kuwa zinamchafua sana licha ya mashabiki kuendelea kumpenda, Madam amebadilika hata katika mavazi yake siku hizi si mnamuona wenyewe!"
Chanzo hicho kilipoulizwa ni kwanini Wema haonekani sana kwenye filamu siku hizi miezi inapita bila kuwa sokoni na filamu yoyote kilijibu "I think ni price yake, waandaaji wengi hawataki kumlipa million 10 anayotaka ili kucheza filamu ya mtu ndiyo maana hayupo tayari kucheza kila filamu"
Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news
No comments:
Post a Comment