Pages

Sunday, August 11, 2013

WASANII WENGI WANA FILAMU NYINGI SOKONI LAKINI AKAUNTI ZAO HAZINA KITU: BATULI

Wasanii wengi nchini wanaonekana kuchoshwa na mikataba mibovu na ya kinyonyaji kutoka kwa wasambazaji wa filamu huku wakiitaka serikali iingilie kati kwa kuweka mikakati mizuri ya kuwasaidia ikiwemo kuweka sheria nzuri za kumfaidisha msanii katika kazi zake. actress maarufu nchini Yobnesh Yusuph(Batuli) anaonekana pia kuchoshwa na hali hiyo na kuamua kuweka wazi kuwa wasanii wengi nchini wana filamu nyingi sokoni lakini akaunti zao za bank hazina kitu huku chanzo mojawapo kikubwa kikiwa ni mikataba mibovu na ya kinyonyaji. Angalia alichoandika star huyo katika twitter....

"wasanii wengi wa filamu huwa tunaamka asubuhi hata hatujui tutakula nini, accounts zetu hazina kitu  wakati tuna films nyingi sana sokoni"

"mikataba ya kazi za filamu Tanzania ukiisoma unaweza ukajuta kwanini uliamua kuwa muigizaji, unauza movie yako na haki miliki kwa miaka 50"

"Wenzetu huamka na mipango kamili ya siku iliyopo lakini wasanii wa films huwa tunaamka huku tukiwaza ni nani wa kumpiga kibomu ili siku iende"

Wasanii wetu wengi ni maarufu na wanakubalika mpaka nje ya nchi lakini kipato chao bado sio cha kuridhisha sababu ya soko la usambazaji kuwa bovu na la kumnyonya msanii hukun serikali ikiwa bado ipo ipo tu na wakati mwingine wanasiasa kuwatumia wasanii kujipigia kampeni ili waingie madarakani lakini wakishapata madaraka wala hawajali tena kuwa kuna wasanii ambao pia huchangia pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi.

Kama wewe ni shabiki wa Batuti basi m-follow hapa kwenye twitter BATULI ACTRESS

Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

7 comments:

  1. Nimetamani kulia pole da Batuli

    ReplyDelete
  2. MASKINI POLENI SISI WATANZANIA HATUJUI WEKENI WAZI TUWASAIDIE WANASHERIA TUPO

    ReplyDelete
  3. Msema kweli adui wa haki

    ReplyDelete
  4. Nakupendaga aunt batuli naomba kujua walau pin yako ya bbm nakuomba aunt batuli nisaidie unaongea point sana

    ReplyDelete
  5. Serikali imekufa vimebaki vyama subirini chadema watawale mtafaidika na sanaa ccm porojo tu

    ReplyDelete
  6. CCM WAONGO MSIWACHAGUE TENA HAWAJATEKELEZA KAZI WALIOAHIDI KWENU

    ReplyDelete