Pages

Wednesday, August 7, 2013

MTOTO WETU ATAITWA TANZANITE SABABU YA UMAARUFU ATAKAO KUWA NAO: FLORAH MVUNGI.

Muigizaji maarufu nchini Florah Mvungi na mumewe H.Baba ambaye pia ni star wa muziki wa Bongofleva na pia muigizaji wa filamu wamekubaliana mtoto wao wanayetarajia kumpata hivi karibuni aitwe Tanzanite hata kama akiwa ni wa kike au wa kiume. Florah amesema kuwa wameamua kumpa jina hilo kutokana na umaarufu atakaokuwa nao mtoto huyo ukichukulia kuwa madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania pekee. Pia amesema kuwa jina la mtoto huyo haliwezi kuingiliana na la mwanamuziki anayeitwa Tanzanite kwakuwa yeye sio jina lake halisi bali mtoto wao litakuwa jina lake halisi. "kama nikijifungua salama awe mtoto wa kike au wa kiume ataitwa jina hilo na atakuwa tofauti sana na msanii wa muziki anayejiita Tanzanite kwa kuwa siyo jina lake halisi bali ni a.k.a tu" alisema Florah akizungumza na GPl.

                                                    Florah Mvungi
Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment