Pages

Thursday, August 15, 2013

Msimu wa ma-miss kuvuma katika filamu umeshapita: Thea

Actress maarufu na mkongwe Swahiliwood Ndumbagwe Misayo(Thea) amesema kuwa ule msimu wa ma-miss kuvuma kwenye tasnia ya filamu umeshapita na waliokuwa wakitamba miaka michache iliyopita kwasasa hawasikiki tena au ni majina tu yamebaki lakini katika filamu hawaonekani tena. miaka Michache iliyopita Thea ambaye ni mmoja wa waigizaji wenye vipaji vya hali ya juu aliwahi kusema kuwa tasnia ya filamu imevamiwa na mamisi ambao wengi wao vipaji hawana. Akizungumza na GPL Thea aliyetamba na michezo kadhaa Kaole na sasa katika filamu alisema "Utabiri wangu unafanya kazi kwa sababu kwa sasa wale wasanii walioibukia kwenye mashindano ya u-miss wengi hawasikiki tena, wasanii wanatakiwa kutambua kuwa sanaa hii siyo lelemama yaani mpaka kufikia hapa tulipo tulifanya kazi ya ziada, tulisota sana kwenye vikundi"

Kwasasa Thea yupo location akishuti filamu mpya akiwa na Jacob Stephen(JB), Shamsa Ford na Bi. Hindu

                                                                Thea
 Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies swp for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment