LuluMsanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana na taratibu zote alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu yake ya “Foolish Age”.Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe pamoja na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo muhimu ya kufanyiwa marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya “Foolish Age” katika Bodi ya Filamu kwa ajili ya ukaguzi. Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni ya Proin Promotions ikiwasilisha filamu yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi.
……………………………………………………………
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
KAMPUNI ya Proin Promotions imewasilisha
filamu yake iliyopewa jina la “Foolish Age” kwa Bodi ya Filamu Tanzania kwa
ajili ya ukaguzi ambapo baada ya kufanyiwa marekebisho filamu hiyo
inaweza kuruhusiwa katika uzinduzi wa Kampuni hiyo hivi karibuni.
Bodi
ilifikia hatua ya kuwaita wahusika yaani Proin Promotions na Elizabeth
Michael (Lulu) kwa ajili ya kufanya majadiliano kuhusu maudhui na
maadili katika filamu hiyo kabla ya kufanyia maamuzi.
Katika
majadiliano hayo Bodi ya Filamu iliwakumbusha wahusika hao kufanya
baadhi ya marekebisho katika filamu hiyo ili iweze kuwa kivutio kwa
umma, pia Bodi ya Filamu iliwakumbusha juu ya umuhimu wa kuzingatia
kifungu cha 14 cha Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ambacho
kinaipa Bodi mamlaka ya kukagua filamu, matangazo na maelezo yote na
kile cha 24 (1) (d, n na t)
cha Kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza kinachofafanua
mambo yanayotakiwa na yale yasiyotakiwa katika filamu ambayo filamu hiyo
imekwenda kinyume. Soma zaidi habari hii HAPA
Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news
No comments:
Post a Comment