Friday, August 30, 2013

ALIYEMJERUHI AUNT EZEKIEL KWA CHUPA NDIYE ALIYEMCHANA LULU KWA VIWEMBE.

 Mtuhumiwa aliyempiga chupa mwigizaji Aunt Ezekiel Jumapili iliyopita nje ya Ukumbi wa Bilicanas ndiye aliyewahi kumchana viwembe mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwaka 2011.
Kwa mujibu wa GPL ni kuwa, mwaka 2011 Lulu alivamiwa na wadada wa mjini baada ya kunaswa katika pozi tata na mwanaume wa watu maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es salaam. Alipoulizwa juu ya sakata hilo, Lulu alisema “Naweza kumkumbuka mwanamke mmoja, namfahamu kwa jina la Yvonne, alinivamia na kuanza kunishambulia huku mkononi akiwa ameshika wembe...”

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Yvonne huyo huyo ndiye aliyedaiwa kumpiga chupa mkononi Aunt ambapo haikubainika mara moja sababu za kufanya tukio hilo.
Aunt alipelekwa katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni na kushonwa nyuzi sita huku mtuhumiwa akishikiliwa na polisi.

                                                            Yvonne
                                               Lulu
Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment