Monday, August 12, 2013

AKI NA UKWA WA BONGO WASAINISHWA MKATABA MNONO.

Waigizaji maarufu Swahiliwood hasa kwa upande wa comedy Nicholaus Ngoda(Ukwa wa Bongo) na Meya Shaban(Aki wa Bongo) wamesainishwa mkataba mnono wa kucheza filamu na kampuni ya International Film Angels ya jijini Dar es salaam ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara mmoja maarufu. Akizungumza na mtandao wa Swahiliworldplanet Ukwa alisema tayari walishaingia mkataba na kampuni hiyo na wanatarajia kuanza kazi na kampuni hiyo ndani ya mwaka huu kabla haujaisha. Pia msanii mwingine Mzee Banana ameingia mkataba kampuni hiyo. Kabla ya hapo  Aki na Ukwa wa Bongo walikuwa wanafanya kazi na kampuni ya Bornagain Film Production.

                                  Nicholaus Ngoda(Ukwa) na Meya Shabani(Aki)
Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies swp for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment