Wakati wa sikukuu watu wengi hupenda kusherehekea hasa kwa kufanya starehe lakini hiyo imekuwa tofauti kwa actress maarufu Swahiliwood Wastara Juma kwa kuamua kutembelea kaburi la mumewe Juma Kilowoko( Sajuki) ambaye pia alikuwa muigizaji maarufu wa filamu na alifariki mwezi January mwaka huu. Wastara alienda katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam lilipo kaburi la Sajuki na kufanya usafi. Wastara alisema "sikukuu yangu nimeitendea haki sana kwa kwenda kuzuru kaburi la mume wangu, Alhamdullilah nimefarijika sana, kimwili siko nae ila atabaki fikrani mwangu". Picha hapo chini inamuonyesha Wastara alipotembelea kaburi hilo juzi Ijumaa
Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies swp
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news
Pole sana mam Mungu yu pa1nawe
ReplyDelete