Tuesday, July 2, 2013

RAYUU AVUTA BANGI ILI KUONDOA STRESS ZA MAPENZI !

Muigizaji wa filamu Rayuu ameweka picha akiwa anavuta sigara na maneno yake kuashiria kuwa anatumia bangi au wengine huita sigara ndefu au kwa kimombo "weed'. Muigizaji huyo aliweka picha facebook na kuweka maneno sambamba na picha hizo kwa madai kuwa anaondoa stress baada ya maisha yake ya kimapenzi kutomuendea vizuri, aliandika "Smoke w.....d" napenda sana, Mapenzi yananitesa zaidi ya inavyonitesa hela"haya mapenzi yataniua" "wat's love, Napunguza stress" Ukiwa na stress kama hivi jidunge tuh""alf nini na nini baadae". Baadhi ya wachangiaji walimlaumu kwa picha hizo na wengine kuchukulia poa tu na hata kumpongeza pia.

Baada ya kuona picha hizo na alichokiandika muigizaji huyo anayependa kujichora tattoo Swahiliworldplanet ilimuuliza kama ni kweli anavuta bangi, alitania au ni picha kutoka filamu yake mpya. Muigizaji huyo alijibu kuashiria ni kweli anatumia lakini baada ya dakika kadhaa akatuma ujumbe wa kukanusha. "Yap, stress zinasababisha haya yote, mtu ninayempenda toka nikiwa mdg nimegundua hanipendi". Baada ya muda kidogo alijibu kwa kukanusha kuwa kuwa hatumii madawa "ctumii madawa bwana" alisema Rayuu

Tungependa kumpa pole kwa kupenda mtu asiyethamini penzi lake lakini kama ni kweli anavuta hayo majani basi hatudhani kuwa ni suluhisho la kuondoa tatizo hilo. Ni wazi kuwa kama anavuta kweli basi anahatarisha maisha yake na hata kazi zake za sanaaa. Tuliza akili yako Rayuu kama ni mapenzi ya dhati utapata atakayekupenda kama kwasasa bado kumpata. Angalia picha hizo..........




No comments:

Post a Comment