Pages

Saturday, July 20, 2013

MUIGIZAJI SALMA JABU(NISHA) KUWAFUTARISHA MASHABIKI WAKE KESHO NYUMBANI KWAKE.

Habari za uhakika ni kuwa muigizaji maarufu Swahiliwood Salma Jabu( Nisha) atafutarisha mashabiki wake wakubwa wa kazi zake za filamu kesho jumapili. Chanzo cha kuaminika kilicho karibu na actress huyo kimesema kuwa mashabiki hao watakaofutarishwa na Nisha nyumbani kwake kijitonyama Dar es salaam watatoka katika group yake ya mtandao wa WhatsApp na tayari kila kitu kipo tayari kwa ajili ya tukio hilo muhimu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Licha ya kuwa actress maarufu Nisha pia ni producer wa filamu kupitia kampuni yake ya Nisha's Film Productions na wiki iliyopita filamu yake mpya ya Tikisa iliingia sokoni. Picha za tukio hilo utazipata hapahapa Swahiliworldplanet.

Mungu akuzidishie Nisha




No comments:

Post a Comment