Star wa filamu za Tanzania Irene Uwoya ametoa
kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake,
Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe,
Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea nchini
Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na Kataut
walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua
kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake.
“Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona
filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka
kusema ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema
Uwoya kwa hasira.
Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu
mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Tanzania akiigiza
filamu na Lucy.
“Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa
karibu angenieleza vizuri kwa sababu hata yeye angeweza kunipigia simu
na kunifahamisha ushiriki wa mume wangu kwenye filamu hiyo kwa kuwa
namba zangu anazo, ilikuwaje hakufanya hivyo?” alihoji.
Kuonesha
kwamba amechukizwa na kitendo hicho, Uwoya alisema kwamba akitua Bongo
atamtafuta Lucy ili aweze kumshughulikia vizuri na ikiwezekana amuoneshe
hiyo filamu waliyoigiza watu wawili tu.
“Nitatua Bongo siku si
nyingi na cha kwanza ni kumtafuta Lucy, anieleze vizuri kuhusu filamu
hiyo waliyocheza na mume wangu,” alisema Uwoya.
Filamu hiyo ambayo
imekuwa maumivu makubwa kwa Uwoya, imechezwa na Lucy na Ndikumana tu
mwanzo hadi mwisho na imepewa jina la "Kwanini Nisimuoe"
credit:globalpublishers
Like our facebook page Swahili World Planet
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.
No comments:
Post a Comment