Wednesday, July 10, 2013

HUU NDIYO UKWELI KUHUSU HABARI ZA MUIGIZAJI JENIFER KYAKA(ODAMA).

Kuna habari na picha zimeanza kusambaa kwenye mitandao  mbalimbali zikimhusu muigizaji maarufu wa filamu nchini Jenifer Kyaka(Odama). Habari hizo zinadai kuwa muigizaji huyo maarufu mara nyingi husema kuwa anakwenda nje ya nchi kikazi zaidi au kununua vifaa vya filamu lakini huwa haendi anakuwa hapa hapa nchini kajichimbia lengo lake ni kutafuta 'kiki" au umaarufu. Baada ya Swahiliworldplanet kusoma habari hizo ilibidi kujaribu kumtafuta Odama kupitia namba zake mbili za kiganjani moja ya tigo na nyingine ya Vodacom ili kudhibitisha kama kweli yupo nchini au lah kwakuwa mara nyingi akiwa nchini hasiti kujibu anachoulizwa. Hata hivyo namba zake zote mbili zimeonyesha hazipo hewani hivyo SWP kulazimika kumuuliza muigizaji mmoja maarufu wa kike ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Odama na tayari walishacheza pamoja filamu kadhaa. Muigizaji huyo alisema kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na Odama yupo nchini Malaysia karibia mwezi na siku 5 sasa "Waongo hao tena wanafik wakubwa odama yupo malaysia kamaliza mwez sasa na cku 5".

Hata hivyo ni jambo la kushangaza kwa madai hayo maana Odama tayari ni muigizaji maarufu ndani na nje ya nchi huku akimiliki kampuni ya filamu. Pia umaarufu wake ukiwa sio wa skendo kama baadhi ya waigizaji wengine bali amejipatia umaarufu kutokana na kazi zake za filamu. Vile vile wakati Odama anaondoka nchini mtandao huu uliweka habari na picha za muigizaji huyo akisindikizwa uwanja wa ndege na ndugu zake na Odama aliandika hivi  "wadau wa filamu safari hii ni ya harakati za kuboresha kazi za kampuni kwa vifaa zaidi na elimu ya utengenezaji filamu za kisasa, kaeni mkao wa kipekee kabisa katika filamu za kampuni yetu zijazo, hakika tunakuja na ulimwengu mpya wa filamu". Kutokana na alichoandika hapo Odama ni wazi kuwa kuna vitu flani anajifunza kuhusu filamu huko Malaysia na akimaliza ndiyo arudi nchini. Hizi ni baadhi ya picha alizoweka katika blog yake wakati anaondoka na nyingine mpya chini ni hizo za photoshop zikimuonyesha akiwa nje ya nchi......

                                            Wakati anaondoka nchini
Aliyedai kuwa Odama yupo nchini ila anajifanya yupo nje ya nchi alitoa picha hizi za Odama kwa mtandao mmoja zikionekana ni za Photoshop, ikionekana Odama yupo nje katika hizo picha. Angalia hapa.............

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates

No comments:

Post a Comment