Pages

Friday, July 19, 2013

HII NDIYO FILAMU YA KWANZA KUSAMBAZWA NA 5EFFECTS BAADA YA KUJITOA STEPS ENTERTAINMENT.

Baada ya William Mtitu ambaye ni muigizaji, muongozaji na producer maarufu Swahiliwood kusitisha filamu za Kampuni yake kusambazwa na Steps Entertainment sasa filamu yake ya kwanza kusambazwa na kampuni yake ya 5 Effects ipo tayari. Filamu hiyo inaitwa Omega Confusion waigizaji wakuu wakiwa ni Kulwa Kikumba(Dude), Irene Uwoya, Mariam Ismail na William Mtitu mwenyewe. Muigizaji huyo wa siku nyingi na ambaye ameshatoa filamu nyingi na kuibua vipaji vingi vipya amewaomba watanzania wasapoti kazi za wasanii wazalendo nchini. " Haya mashabiki wetu....tunaingiza kwa mara ya kwanza sokoni filamu ambayo itasambazwa na 5Effects movies...weka historia kwa kusapoti kampuni ya kizalendo inayomilikiwa na watanzania wenzako, tunakuahidi hatutokuangusha, tunaingiza kwa mara ya kwanza bonge la filamu...OMEGA. Kuwa sehemu ya historia kwa kujipatia nakala yako" alisema Mtitu.

Hongera 5Effects kwa kuanza kusambaza filamu wenyewe kwakuwa ni moja ya hatua nzuri kuzidi kuendeleza tasnia ya filamu nchini.


No comments:

Post a Comment