Pages

Wednesday, July 10, 2013

BATULI, RIYAMA ALLY, BABA HAJI KUTIKISA NA FILAMU YA OUR HOLY MONTH OF RAMADHANI MWEZI HUU.

Filamu mpya ya "Our Holy Month Of Ramadhan" itaingia sokoni katikati ya mwezi huu wa ramadhani na itasambazwa na kampuni ya Leo Media. Filamu hiyo imeandaliwa na Yobnesh Yusuph(Batuli) ambaye pia ni mmoja wa waigizaji wakuu ndani ya filamu hiyo. Tayari wadau na mashabiki wa filamu za kiswahili wameanza kuiulizia wakijua tayari imetoka lakini habari za uhakika ni kuwa inaingia sokoni katikati ya mfungo huu wa Ramadhani. Ukiachilia mbali Batuli mastaa wengine katika filamu hiyo ni Riyama Ally, Haji Adam(Baba Haji), Hidaya Njaidi, Suleimani Barafu, Thecla Mjata, Swebe na wengineo. Usikose kununua nakala halisi itakapotoka ili kukuza sanaa ya nyumbani


No comments:

Post a Comment