Tuesday, June 25, 2013

TUZO ZA AFRICAN FILM DEVELOPMENT AWARDS 2013 ZASOGEZWA MBELE.

Tuzo za African Film Development Awards(AFDA) 2013 zilizokuwa zimepangwa kufanyika June 29, 2013 zimesogezwa mbele mpaka tarehe 31 August mwaka huu kutokana na sababu kadhaa zikiwemo ujio wa rais Obama. Hayo yalisemwa na mwakilishi wa tuzo hizo nchini bwana Mnyela alipotafutwa na Swahiliworldplanet baada ya watu kutokuwa na uhakika kuwa zitafanyika tarehe iliyopangwa mwanzoni au la!. Alisema "Tuzo zimeahirishwa na sasa zimepagwa kufanyka 31st August 2013 hapa DSM sababu ni ugumu wa logistics za accommodation ya wageni wetu kwasababu ya ujio wa Obama, Zuma na mkutano mwingine mkubwa, ila tarehe 7 July 2013 kutakuwa na Pre-awards party itakayofanyika Zanzibar kwenye platform ya ZIFF". Tuzo hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na mastaa na wadau kadhaa kutoka ndani na nje ya bara la Afrika.

Hata hivyo kuna baadhi ya sintofahamu kutoka kwa wadau wa filamu nchini hivyo Swahiliworldplanet haikusita kumuuliza Mr. Mnyela ili wadau wa filamu wapate majibu na kuondokana na wasiwasi. Kwanza ni baadhi ya wadau kunong'ona chinichini kuwa Clouds Entertainment ambayo ndiyo imepewa jukumu la kuandaa event hiyo hapa nchini haina nia ya dhati kuzitangaza tuzo hizo(publicity) ili wadau wajue hivyo kupelekea mwamko mkubwa siku ya tuzo hizo kwa wadau wengi nchini. Inadaiwa kuwa Clouds wana mpango wa kuwa na tuzo zao za filamu na muziki nchini hivyo sio rahisi sana wao kutoa mkazo unaotakiwa katika AFDA. Mnyela alitoa ushirikiano kwa kujibu "ninadhani hiyo haina ukweli, hizi ni tuzo za Afrika(kimataifa) bila shaka utagundua intended audiences yetu ni tofauti kabisa na ikiwa clouds watafanya tuzo zao ambapo sina uhakika kama nazo zitakuwa za kimataifa au za local. Kwa kifupi sisi kama foundation hatuna shaka na u-weledi wa clouds ambao si media partners tu bali ndo event's manager".

Pia baadhi ya wasanii wanaonekana kutokujua namna ya kupata mwaliko wa tuzo hizo hivyo wengine kuuliza SWP kuhusu namna ya kupata mwaliko ili kuhudhuria tuzo hizo zinazotarajiwa kuitangaza zaidi film industry ya Tanzania nje ya nchi. Mr. Mnyela alitolea ufafanuzi kwa kujibu "kuhusu mwaliko hayo tutayaweka bayana tena pindi muda utakapofika, hopefully umeelewa majibu yangu vizuri".

We wish the whole team of AFDA all the best



No comments:

Post a Comment