Wednesday, June 26, 2013

MUIGIZAJI SUZANA LEWIS(NATASHA) AFUNDWA.

Muigizaji mkonge na maarufu nchini Suzana Lewis(Natasha) juzi alifundwa au kupewa nasaha mbalimbali za maisha ya ndoa ikiwa ni moja ya hatua kuelekea kufunga ndoa na mumewe mtarajiwa. Sherehe hiyo ya kumfunda ilifanyika Tandika maghorofani jijini Dar es salaam ikiwa imeandaliwa na rafiki yake wa karibu aitwaye Nuru. Mastaa kibao walitoa sapoti kwa muigizaji huyo ambaye ni mama mzazi wa Yvonne Cheryl(Monalisa) ambaye pia ni actress maarufu Swahiliwood. Wahudhuriaji walivaa kiasili huku wakiwa na furaha tele. Baada ya hapo msafara wa shamra shamra hizo ulielekea Yombo ambako ndiyo nyumbani kwa Natasha aliyetamba na filamu kibao. Natasha mwenyewe alisema "nashukuru sana jamani kwa kupita hatua hii ya kwanza kuelekea kwenye ndoa yangu, Siwezi kuacha kumshukuru zaidi rafiki yangu Nuru kwa kunifanikishia".
 

                   image by www.globalpublishers.info


No comments:

Post a Comment