Monday, June 17, 2013

JACKLINE WOLPER NA MH.HALIMA MDEE WAJIFUA VILIVYO KWA AJILI YA PAMBANO LAO LA NGUMI(PHOTOS)

Actress Jackline Wolper anajifua vilivyo kwa ajili ya maandalizi ya pambano lake la ngumi na Mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee katika Tamasha la Matumaini litakalofanyika tarehe 7 mwezi ujao. Wolper anajifua akiwa Dar es salaam wakati Halima Mdee anajifua huko Dodoma chini ya Mh. Idd Azan ambaye pia siku hiyo atapanda ulingoni kupambana na Jacob Stephen(Jb) ambaye ni actor maarufu Swahiliwood. Halima Mdee ametamba kumchakaza Wolper huku Wolper nae akijipanga vizuri ili kumuonyesha Mdee kuwa yeye yupo fit. Mwaka jana katika Tamasha hilo Wolper alipambana na Wema Sepetu na kuonyesha uwezo mzuri kuliko Wema. Angalia picha...............

              Mh. Halima Mdee
Images by www.salehejembe.blogspot.com

No comments:

Post a Comment