Pages

Saturday, June 15, 2013

HONGERA DR.CHENI KWA PERFORMANCE NZURI.

Filamu ya Majanga(Disasters) ilitoka miezi kadhaa iliyopita lakini baada ya kuingalia zaidi ya mara mbili imebidi kuandika hapa ili kumpongeza muigizaji mkuu wa filamu hiyo Muhsin Awadhi(Dr.Cheni) kwa jinsi alivyofanikiwa kuuvaa vizuri uhusika wake. Filamu hii imeshirikisha waigizaji wengi chipukizi lakini ningependa tu kugusia uigizaji wa wa Dr.cheni. Kwanza kabla ya yote character yake iliendana vizuri na muonekano wake kama kijana mwenye mvuto na muonekano wa kitanashati huku akiwa  na pozi kama kijana aliyetekwa na tamaduni za kimagharibi sana. Pili na ambalo ni muhimu zaidi alifanikiwa kuubeba uhusika vizuri kama kijana wa kisasa anayejikweza kwa kujifanya ana pesa na familia yake ni tajiri kumbe ni kinyume. Muda mwingi anaazima nguo kwa watu au kwenye maduka ili watu hasa wasichana anaojihusisha nao kimapenzi wajue ni mtu anayejiweza kimaisha.

Waigizaji wengi katika hii filamu walicheza vizuri lakini kivutio hasa alikuwa Dr. Cheni kwa kuuvaa vizuri uhusika wake uliokuwa na mbwembwe nyingi na kufanikiwa kumkaa vizuri. Filamu imeegemea zaidi katika upande wa comedy lakini bado Dr. Cheni alijitofautisha kama muigizaji serious katika nafasi ya comedy. Uchezaji wake ulikuwa tofauti na hawa wachekeshaji uliowazoea ila yeye katika filamu hii anakuchekesha na pia amefanikiwa vizuri kuufikisha ujumbe kwa hadhira. Generally this is one of his best performances to date na amedhihirisha kuwa kipaji anacho kiasi cha kuweza kucheza vizuri katika uhusika wa aina yoyote. Kama hujaiona filamu hii itafute utacheka na kuburudika kutokana na vituko vya wahusika.


No comments:

Post a Comment