Actress Zamda Salum amesema kuwa kwa sasa ana safari za kibiashara nje ya nchi kila kukicha ndiyo maana spidi yake katika filamu imepungua lakini akitulia ataliendeleza libeneke la filamu kama kawaida. Zamda ambaye huko nyuma ametamba na filamu nyingi na nyingine akiwa na marehemu Steven Kanumba amesema kuwa kwasasa hakai sana Bongo kwakuwa anafanya biashara katika nchi za Thailand na Turkey. Zamda aliyasema hayo alipoulizwa na Swahiliworldplanet ni kwanini kwa sasa hayupo active kwenye movies na kujibu "saiv sipo tz kwa sana ni mtu wa safar kila kukicha, but sio kama nimeacha....nikishatulia nitaendelea kama kawaida.". Zamda amesema kuwa anafanya biashara ya nguo za kike, nywele na vitu vingine na duka lake linaitwa Zamda Trends na lipo Mbezi beach njia ya chini jijini Dar es salaam. Actress huyo mwenye mvuto alipoulizwa tena kama ana mpango wa kufungua kampuni yake ya films kwa kuja na vifaa vya kutengenezea filamu alijibu "inshaallah tuombe uzima".
No comments:
Post a Comment