Pages

Wednesday, May 22, 2013

MTOTO WA BATULI KUONYESHA CHECHE ZAKE SWAHILIWOOD.

News is that Jaheim ambaye ni mtoto wa actress maarufu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) soon ataonekana katika filamu ambayo inaandaliwa na Batuli mwenyewe. SWP ilipomuuliza batuli kuhusu hilo alisema "Katika film yng ninayotarajia kuianza ndipo ataanza kuonekana humo". Jaheim anaungana na mtoto wa actress Chuchu Hans anayeitwa Farihiya ambaye kuna filamu inakuja ameigiza na Chekibudi, Johari na wengineo. Tayari kuna baadhi ya mastaa wa Swahiliwood wanaotamba sasa ambao walianza kuwa mbele ya kamera tangu utotoni kama mastaa wengi wa nje pia walivyo. Acha tusubiri ujio wa Jaheim kama ataweza kukubalika haraka kwenye movies kama mama yake ambaye anatamba kwasasa kwenye movies mbalimbali kama vile Kazi Yangu, Waves of Sorrow na nyinginezo. Pia filamu kadhaa za Batuli zinakuja ikiwemo Coast To Coast akiwa na Slim Omar.

                                                                Jaheim
                                             akiwa na mama yake

1 comment:

  1. Napenda hii blog sana bt tuwekee majibu ya maswali haya batuli kazaa na ray?

    ReplyDelete