Friday, May 31, 2013

MAMA MZAZI WA ACTRESS FLORAH MVUNGI AKATAA MWANAE KUFANYIWA KIBAOKATA AKISEMA NI UFUSKA.

Zuhura Mvungi ambaye ni mama mzazi wa actress maarufu Florah Mvungi amekataa mwanae kufanyiwa kibaokata kwa madai ni uhuni na pia ni kinyume na maadili ya mtanzania na akasema kama kitafanyika atagomea ndoa. Kibaokata kilitakiwa kufanyika jumamosi iliyopita nyumabani kwa msanii Salma Jabu(Nisha) lakini hakikufanyika baada ya mama mzazi wa florah kukataa kwa kusema ni ufuska. Flora mwenyewe alipoulizwa na www.globalpublishers.info kuhusu hilo alisema "mama alikataa nisifanyiwe kibaokata akidai ni ufuska hivyo anataka nifanye vitu vinavyoendana na maadili". Florah na H.Baba wanatarajia kufunga ndoa tarehe 8 mwezi wa 6 mwaka huu huku tayari muigizaji huyo akidaiwa kuwa mjamzito.


No comments:

Post a Comment