Pages

Tuesday, April 30, 2013

"NAIROBI HALF LIFE" MOJA YA FILAMU NZURI ZA KISWAHILI BARANI AFRIKA.

Nimeangalia filamu ya Nairobi Half Life(2012) juzi na Jana nikiri tu kuwa ni moja ya filamu chache nzuri zilizowahi kutengenezwa kwa kiswahili barani Afrika na hata nje ya Afrika. licha ya kuwa na story ya kawaida but imeandikwa vizuri na climax ya hii filamu mtu yeyote haikuwa rahisi kutarajia ingeishaje kitu ambacho pia kimeifnya iwe tofauti kwa kiasi chake. Mwanzo mpaka katikati ya hii filamu ipo kawaida lakini kuanzia kati kuendelea inakufanya utake kuangalia zaidi nini kitatokea. Filamu hii imetengenezwa Kenya ikitumia lugha ya kiswahili huku ikiwa imeongozwa na David Tosh Gitonga na mhusika mkuu akiwa ni Joseph Wairimu kijana mwenye muonekano wa kawaida sana lakini akionyesha kipaji cha kuigiza. Joseph wairimu ameigiza kama kijana anayeuza dvd za filamu za kimapigano kutoka nje na katika biashara yake hiyo anaigiza vitendo vya hao waigizaji maarufu wa Hollywood akiwa na ndoto ya kuwa muigizaji maarufu. Anawaaga wazazi wake kutoka kijijini ili aende Nairobi kutimiza ndoto yake ya kuwa muigizaji maarufu lakini huko anakutana na vizingiti kibao na vibweka vya majiji mengi kama ilivyo kawaida. Hatimaye anaingia katika genge la vijana wenzake ambao hufanya kazi za kupora na kuibia watu ili waishi. Taratibu na yeye anakuwa mzoefu katika wizi mpaka kufikia kuiba magari lakini ndoto yake ya kuigiza ikiwa pale pale.

Hii filamu ilipita katika hatua ya kwanza katika Tuzo za Oscar mwaka huu ingawa haikufanikiwa kupita hatua ya mwisho kwenye kipengele cha Best Foreign Language Film. Katika tuzo za African Movie Academy Awards(AMAA) ilichaguliwa kushindania tuzo katika vipengele tisa. Kizuri zaidi katika hii filamu ni location zake huku picha za filamu zikiwa nzuri sana na waigizaji nao wakiwa poa. Muongozaji alifanya kazi nzuri sana hata hivyo kuna scene moja Mwas(Joseph Wairimu) anapigwa chupa ya kichwani huku chupa hiyo ikipasuka vipande vipande lakini hakuonekana kuwa na jeraha akiwa ameanguka chini na kuinuka ghafla pasipo kuonyesha vizuri hisia za kuumia na majeraha, hapa palikuwa na kosa kidogo ingawa siyo rahisi kugundua. Kwa ujumla ilikuwa chaguo zuri kuitengeneza filamu kwa lugha ya kiswahili ili Afrika mashariki iwe na utambulisho wake katika ulimwengu wa filamu. Hii filamu pia ilionyeshwa katika majumba kadhaa ya filamu nchini Marekani. Hongera kwa watengenezaji wa Nairobi Half Life.

                                                  Joseph Wairimu in the movie

No comments:

Post a Comment