Monday, April 29, 2013

FILAMU YA CRAZY IN HOSPITAL SIO YA KUKOSA: NICHOLAUS NGODA

Nicholaus Ngoda muigizaji machachari wa Swahiliwood hasa katika comedy amesema kuwa filamu mpya ya Crazy in Hospital ni moto wa kuotea mbali maana wamefanya makubwa humo ndani shabiki anaweza kucheka mpaka basi. Pia amesema wamezingatia maadili ya kitanzania na kiafrika kwa ujumla. "Kaka Crazy In Hospital ni zaidi ya movies tulizowahi kucheza hapa Tanzania utacheka hadi utoe haja ndogo hapo hapo". Filamu hiyo inaingia sokoni muda si mrefu. Katika filamu hiyo waigizaji wakuu ni Zawadi, Novatus Mayenja, Nicholaus Ngoda na Meya Shabani ambao wote kwa pamoja hufananishwa na Aki na Ukwa wa Nollywood. Filamu imetengenezwa na Bornagain Film Production chini ya Emanuel Myamba(Pastor Myamba) Usikose filamu hiyo kwa ajili ya kuburudika na familia yako.




No comments:

Post a Comment