Actress Matumaini ameiomba
serikali imsaidie kupata matibabu ili aweze kupona maradhi ya figo na
ini yanayomkabili.
Akizungumza na www.globalpublishers.info alisema: “Hali
yangu bado si nzuri ingawa natumia dawa lakini sijapata tiba sawasawa.
Sina fedha na familia yangu kwa sasa imeishiwa kwa sababu magonjwa
yanayonisumbua ni makubwa na yanahitaji fedha nyingi.
“Naiomba serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na
Michezo isikie kilio changu. Hali yangu si nzuri, nahitaji msaada ili
kuokoa maisha yangu. Nina imani nikipata tiba kamili nitapona na
kurejea tena jukwaani.”. Tunakuombea upone haraka Matumaini
source: www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment