Thursday, March 7, 2013

ACTORS WA SWAHILIWOOD WANAOVAA ILI WAPENDEZE KATIKA FILAMU NA SIO KUTOKANA NA CHARACTER

Kama mtu niliyesomea costume designing for the stage and the screen huwa nasikitika sana kuona filamu zetu  zikiwa na tatizo kubwa katika kipengele cha costumes ambacho ni muhimu sana katika tasnia hii na ndiyo maana vyuo vikuu vinafundisha mpaka shahada ya pili na hata ya tatu ya costume for films,theatre and Tv. Filamu za kitanzania hakuna kitu kinachoitwa costumes and nimeuliza baadhi ya actors wamenambia huwa wanaenda na mavazi yao kwa kuwa producers hawana bajeti ya costumes..shame on you Tanzanian film producers!. Ukweli ni kuwa bajeti hata ya laki 3 mpaka 5 inatosha kwa ajili ya mavazi stahili katika baadhi ya filamu zetu kutokana na utafiti niliofanya hata hivyo uvivu na hulka ya kulipua kazi ndio sababu. Kwa kuwa tatizo hili ni kubwa sana kiasi cha kuharibu story za filamu kibao licha ya kuwa nzuri wakati mwingine  basi tuangalie waigizaji hasa wakuu ambao mara nyingi  mavazi yao hayaendani kabisa  na uhusika wanaocheza.au tuseme wanavaa tu ili wapendeze wakati mwingine bila kujali character inataka nini. Hata hivyo tatizo hili linachangiwa pia na directors maana haiwezekani director umuongoze msanii katika uhusika flani wakati mavazi, make up na muonekano wake kwa ujumla haviendani na character husika. Pia make up inahusishwa hapa kwakuwa huenda sambamba na mavazi aghalabu. Waigizaji wafuatao ni mfano mzuri kwa kuvaa mavazi yasiyoendana na character katika filamu zao nyingi licha ya kuwa wapo wengine lakini hawa ni mfano hai.

HEMEDY SULEIMAN
Licha ya kuwa uigizaji wake unatia shaka sana lakini pia mavazi yake mara nyingi anaonekana kuigiza zaidi ya kuigiza. mara nyingi filamu zake kavaa vipuli, akiwa kalala, bafuni, ofisini mwanzo mpaka mwisho na kuonekana kama mtalii ndani ya filamu na siyo actor.

IRINE UWOYA.
Filamu nyingi alizocheza uwoya mavazi ni zero katika kuendana na na uhusika, mtu yupo ofisini kavaa nusu uchi au gauni la mpira au nguo za kutokea usiku. Filamu ya OPRAH ikiwa moja ya mifano mizuri. Hata make up zake huwa haziendani na uhusika mara nyingi, kope za bandia, kucha, tattoo zake kifuani zinaonekana katika uhusika usistahili.

VICENT KIGOSI(RAY)
Matatizo mawili makuu yanayoharibu filamu zake ni kushindwa kucheza na sauti yake na pia mavazi. Mara nyingi anavaa ili apendeze na siyo kwa ajili ya uhusika. Mtu ni bosi katika ofice ya kisomi na yenye hadhi kubwa lakini kavaa vipuli muda wote na kutoka mwanzo wa filamu hadi mwisho. mtu yupo ofisi ya hadhi ya kipekee kavaa jeans au suti za usiku, kofia za zisizostahili.Mtu anaigiza kijijini na maisha magumu ajabu lakini nywele zinawaka wave na kuwekwa mitindo ya kisasa. Mfano mzuri angalia filamu ya SURPRISE, WAVES OF SORROW, MY DREAMS,OPRAH, WOMAN OF PRINCIPAL na nyinginezo.
JACKLINE WOLPER
Mara nyingi mitindo yake ya nywele kucha na mavazi haviendani na characters anazocheza. ofisini kavaa nguo za usiku au za kawaida tena zenye rangi za kuwaka ajabu. Mfano mzuri angalia filamu yake ya STUCK ON YOU, SURPRISE na nyingnezo. inakuwa too much kiasi cha kuharibu uhusika
SALMA JABU(NISHA)
Licha ya kwamba mara nyingi anakuwa na overacting lakini pia mavazi, nywele na mapambo kwa ujumla mara nyingi vinashindwa kuendana na uhusika anaocheza. Anapenda sana kuvaa nywele zenye rangi kali kiasi cha kukosa point yoyote ile. kope na wanja mpaka basiiiiiiiiii!. mwangalie katika PUSY NA PAKU na filamu nyingnezo.
WEMA SEPETU
Hawezi kuondoka hapa hata kwa dawa, katika filamu zake nyingi tatizo hili limejitokeza. Mfano hai ukiwa katika filamu yake ya IT WAS NOT ME akiwa amecheza kama mwanafunzi wa chuo kikuu nywele zina rangi kali mwanzo mpaka mwisho wa filamu tena za aina moja licha ya kuwa na uwezo wa pesa kiasi cha kusaidia wengine katika fiilamu. mbaya zaidi mwanafunzi wa chuo kikuu eti ana tattoo shingoni na muda wote yaonekana! chuo kikuu gani hicho Tanzania!
FLorah Mvungi
Nae pia mavazi na nywele zenye rangi, kali kucha muda wote hata sehemu zisizostahili

ELIZABETH MICHAEL(LULU)
Filamu nyingi kacheza licha ya kuwa na kipaji na kufanikiwa kuuvaa uhusika mara nyingi lakini mavazi huwa nje ya point. Mfano mzuri angalia filamu ya HOUSE BOY, nywele na mavazi mhh..
AUNT EZEKIEL
Filamu zake nyingi tatizo hili limejionyesha waziwazi
JACKLINE PENTEZEL
Katika filamu zake nyingi pia mavazi hayaendani na uhusika anaocheza.




No comments:

Post a Comment