Pages

Sunday, February 3, 2013

TUZO ZA AFRICA MAGIC BADO HAZINA UMUHIMU MKUBWA KWA FILAMU ZA KITANZANIA

Hivi karibuni nominees kwa ajili ya tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards 2103(AMVCA) walitajwa lakini ukiangalia nominees na tuzo hizo kwa ujumla nl kuwa zimetoa kipaumbele kwa asilimia kubwa kwa filamu zinazotengenezwa kwa lugha ya kiingereza pekee hivyo kuifanya South Africa, Nigeria na Ghana kutawala katika tuzo hizo. Nchi zinazotengeneza filamu kwa lugha za kiafrika hazikupewa sana kipaumbele badala yake zimewekewa category moja maalum kwa ajili ya filamu za lugha husika kushindana zenyewe kwa zenyewe hivyo kuonyesha kwa urahisi kuwa waigizaji wa Tanzania hawawezi kuwekwa pamoja na waigizaji wa nchi nyingine katika categories za best actor na best actress achilia mbali categories za best film na best director. Hii imeonyesha kuwa tuzo hizo hazina uzito wowote kwa ajili ya filamu za kitanzania kwa kuwa filamu zetu zinatumia zaidi kiswahili. Hivyo kuna kila sababu ya Tanzania kuwa na tuzo zake za filamu na siyo kutegemea tuzo hizi hata kidogo, Kiingereza siyo kigezo cha filamu kuuuzika kimataifa au filamu kuwa bora na kama ni hivyo India isingekuwa tishio kwa Hollywood.Filamu chache za kitanzania zinaweza kutengenezwa kwa kiingereza kutokana na matakwa ya mtengenezaji ila kutumia kiswahili ni uamuzi mzuri zaidi kwa kuwa lugha hii ni ya kimataifa,subtitles ziwekwe kwenye filamu zetu huku tukiendelea kujifunza kupitia elimu ya filamu ili kufika mbali zaidi.Ahsanteni

No comments:

Post a Comment