Pages

Wednesday, February 13, 2013

SHAMSA FORD AWAZODOA WANAOSEMA AMEPOTEZA MVUTO

Actress Shamsa Ford from Swahiliwood amesema kuwa, wanaosema  amepoteza mvuto baada ya kujifungua wanakosea sana kwani ndiyo kwanza amezidi kuwa na mwonekano mzuri. Shamsa alisema: “Siamini kama kuzaa kunasababisha kupoteza mvuto lakini hata kama ndivyo basi kwa upande wangu hilo halijatokea. Ndiyo kwanza nimezidi kuwa na mvuto.”
Alienda mbali zaidi kwa kueleza kuwa kilichomsaidia zaidi kuongeza mvuto wake ni mazoezi na kuzingatia urembo. “Asikudanganye mtu, hata kama hujazaa, mwanamke lazima azingatie masharti ya urembo na mazoezi ya mwili ili kuufanya mwonekano kuwa wa kuvutia, ndiyo maana unaniona hivi,” alisema Shamsa na kuongeza: “Nadhani ndiyo sababu hata baba mtoto wangu (Dikson Matoke) ameongeza mapenzi kwangu, ni kwa sababu ya kujitunza,  amekuwa akiniambia waziwazi kuwa mvuto wangu kwa sasa ni mzuri zaidi.”

                                                                 credit:globalpublishers.com

No comments:

Post a Comment