Siku za hivi karibuni muigizaji Vicent kigosi maarufu kama Ray ameingia katika mtafaruku na mapadri wa kanisa katoliki kwa madai kuwa filamu yake mpya ya Sister Marry inadhalilisha kanisa katoliki kwa matendo yaliyoonyeshwa katika filamu hiyo ambayo siyo ya kweli kwa mujibu wa viongozi hao wa kidini. Binafsi sijaiona filamu hiyo kwakuwa bado haijatoka lakini katika mtifuano huo kunaonekana kuwa na kasoro kubwa hasa katika kulifuatilia,kulishughulikia na hatimaye kulimaliza suala hili.imeandikwa
kwenye vyombo vya habari kuwa Ray aliambiwa na mapadri wa kanisa katoliki aandike barua ya kujieleza kuhusu filamu hiyo na kabla hajaandika aliitwa kwenye kikao kilichojumuisha mapadri 4, mtu mmoja anayedaiwa kutoka usalama wa taifa na mtu mwingine aliyedaiwa kutoka ofisi ya utamaduni jina lake ni Mwansoke na ilidaiwa mpaka mwisho wa kikao hakukuwa na mwafaka wa kikao hicho kwa Ray kuambiwa na mapadri afute vipande walivyovigunia na wengine kusema filamu isipelekwe sokoni kabisa hivyo Ray kuwa njia panda hasa kutokana na pesa kubwa iliyotumika kuandaa filamu hiyo. hembu tuangalie sasa suala hili............
Kwanza kabisa, nilistaajabu kwa mwakilishi yoyote au bodi ya filamu
kutotajwa kuwepo kwenye kikao, au huyo mtu aliyedaiwa kutoka ofisi ya
utamaduni ndiye alikuwa mwakilishi wa bodi ya filamu na kama ni kweli
mbona sasa haikuwekwa wazi kama yeye ndiyo alikuwa mwakilishi!.Suala
hili la filamu ya Ray linaonyesha waziwazi udhaifu uliopo katika bodi ya
kukagua filamu na hata viongozi wengine katika taasisi zinazoshughulikia sanaa. Kabla ya kuingia sokoni
bodi ya filamu ndiyo inatakiwa kuikagua filamu na kuizuia irekebishwe
katika baadhi ya vipande, kuiwekea madaraja au kuiruhusu iingie sokoni
na siyo mtu binafsi au kikundi cha watu au taasisi nyingine kwani bodi
ya filamu huwa ni chombo kilicho chini ya serikali mara nyingi. Hivyo
bodi ilitakiwa kuwa msemaji mkuu na mwenye nguvu katika suala hili
huku ikisikiliza madai na malalamiko yote kutoka pande zote
mbili lakini imekuwa kinyume badala yake viongozi wa dini kuwa wasemaji
wakuu na kuonekana kutawala kikao hicho.vile vile mtu huyo kutoka ofisi
ya utamaduni alikaririwa hapo hapo kikaoni akisema vipande vyote
vilivyoguniwa vinyofolewe! Tumesikia filamu bado hata kuingia sokoni je
viongozi hao wa dini wamekuwaje na nguvu ya kiasi hicho kuliko hata bodi
iliyoundwa kwa ajili ya kazi hiyo kama siyo udhaifu wa wazi wazi wa utendaji wa chombo hicho!
Pili,
ni sawa kufuta baadhi vipande katika filamu lakini inatakiwa kuangalia vipande hivyo kwa undani zaidi. simtetei Ray hapa naomba ieleweke ila kuliangalia suala hili kwa undani kidogo maana naheshimu dini ya kila mtu. Kama viongozi wa dini wamekuja na kutaka vipande hivyo vinyofolewe na
mwakilishi wa ofisi ya utamaduni kuridhia itakuwaje makundi mengine
katika jamii ambayo huwa yanaguswa katika filamu kwa kuelezewa upande
mbaya(negative side)kama vile majambazi,wala rushwa na hata machangudoa
kutaka vipande vinavyoonyesha tabia zao vifutwe, ofisi ya utamaduni pia
itaridhia.Tunasikia kuwa viongozi hao waliulizwa kuwa vipande gani
hawajavipenda ili viondolewe. Je viongozi hao wa dini wamesahau kuwa
kilichofanyika ni sanaa na siyo lazima tabia hiyo iwe kutoka kanisa
katoliki au waumini wake. viongozi hawa hawakuulizwa kuwa wanafikiri
kila muumini au kiongozi wa dini ni msafi ?. Niseme tu kuwa viongozi hao
wa dini walikuwa na haki ya kuangalia filamu hiyo na hata kutoa
mapendekezo yao lakini wanatakiwa wajue kuwa kuna watu wachafu pia
katika nyumba za ibada licha ya kuonekana wasafi machoni hivyo msanii
hakulilenga kanisa hilo bali alijaribu kutaka kufikisha ujumbe tu kwa
jamii nzima bila kujali dini ya mtu. Ikumbukwe kuwa viongozi wa dini
husisitizia waumini wao wawe na maadili mema lakini kabla baadhi ya
waumini kufika katika nyumba za ibada ujumbe huo unaweza kupatikana au kuwafikia hata kupitia
sanaa ikiwemo filamu wakiwa majumbani kwao. Si lazima viongozi wa
dini wawe wameyaona yaliyoonyeshwa kwenye filamu hiyo kwani hata baadhi
ya waumini wao wanaweza kuwa walishawahi kuyaona mahali au kusimuliwa.
Pia msanii anaweza kupewa wazo la stori na mtu ambaye aliwahi kushuhudia
matendo hayo siyo lazima yawe katika kanisa hilo bali yanaweza kutoka katika dhehebu lolote lile.
Tatu, kutokuwepo kwa wachambuzi wa filamu(film critics) katika filamu za kitanzania nako kumejitokeza hapa. Film critics ni watu muhimu sana katika tasnia ya film ulimwenguni kote lakini hapa kwetu mpaka sasa hawaonekani na kama wapo basi bado kujitokeza. Nasema hivyo kwasababu critics wanaweza kuivamia au kuipongeza filamu, hivyo katika suala la Ray wao pia wangetoa mchango wao hata kama industry yetu bado kukua, miaka 10 sasa tangu tasnia hii ianze rasmi si haba kwanini wasijitokeze film critics mpaka sasa!. Ray anaonekana kukosa sapoti hata kutoka kwa baadhi ya wasanii wenzake maana hakuna shaka kuwa wapo wanaochekelea kwa kilichomkuta . Wahenga wanasema mwenzako akinyolewa wewe tia maji! Kama yametokea kwa Ray basi hata watengeneza filamu wengine yatakuja kuwakumba katika filamu zao huko mbeleni. Hata kama Ray ana makosa katika filamu yake lakini wasanii wanatakiwa kuonyesha umoja katika suala hili hasa kuhusu utendaji wa bodi ya filamu ili kuwe na taratibu nzuri za kueleweka kuhusu ukaguzi wa filamu na hata filamu ikizuiliwa au vipande kufutwa basi iwekwe wazi na bodi hiyo ni jinsi gani msanii hapati hasara au atalipwaje gharama zilizotumika. Nasema hivyo kwa kuwa tasnia hii inakuwa na itakuja kufikia hatua ambayo kutakuwa na story nyingi za kuonyesha uovu au uzo wa baadhi ya taasisi zikiwemo za kiserikali au binafsi.
N.B : Makala hii fupi ilitakiwa kutoka mapema lakini ilichelewa kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu. Tuendelee kupeana maoni na mawazo ili kuijenga tasnia hii ya filamu nchini. Ahsanteni
Mimi ndhani hapa cha umuhimu ilikuwa wewe kuandika kama report yaliyomkuta Ray maaana kama haijatolewa taarifa juu ya kile kinacholalamikiwa na hao viongozi wa dini. Nimesoma na mimi huwa mvivu kusoma makala ndefu kidogo. Nimevutiwa na jinsi ulivyoandika maana nilikuwa na.matumaini ya kupata kiini cha hicho.kitu. Na sidhani kama ni vema kuandika kama hivi wakati habari kamili juu ya hivyo vipande vinavyolalamikiwa hajajulikana. Mimi natoa maoni haya maana. kwanza najua kila dhehebu lina utamaduni.wake. mfano jinsi ya matendo yanayofanywa na biongozi na wini wakati wa kuabudu kanisani . Pia kama kuna.ugomvi ndani ya nyumba wanazoishi pia kuna jinsi ya taratibu za kufuata. na hapo mwandishi anaweza cheza na migogoro kwa mlolongo mzima. Pia sister hadi awe suster kamili.kuna jinsi ya uvaaji nk. Hata hivyo pia wana kiongozi wao.
ReplyDeleteMimi ningependa ufuatilie tena zaidi iliutujuze juu ya kile kinachowakera viongozi wa hili dhehebu na hapo sasa sisi kama wasaniii tuone.ni.jinsi.gani.uhuru wetu unaingiliwa na tutawezaje kujitetea pindi tutakapo kumbana na hayo.
Asante.kwa kutujuza juu ya hali filamu ya Ray.
Nawakilisha.