Pages

Friday, February 22, 2013

MUIGIZAJI LULU AKUBALI KURUDI SHULE KUENDELEA NA MASOMO

 Actress Elizabeth Michael(Lulu) ajipanga kujiendeleza  kimasomo ili aweze kupambana na changamoto za maisha.
Akizungumza na Maisha msanii wa filamu Dk. Cheni amebainisha kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa kurudi shule ili aweze kuendelea na masomo yake na hata familia yake inataka aendelee na masomo lakini familia haina uwezo wa kulipia gharama za masomo yake kwa sasa.
Dk. Cheni aliweka wazi kuwa kutokana na kipato cha familia ya actress huyo anatakiwa kwa sasa aweze kufanya kazi yake ya filamu ili aweze kujimudu kama ilivyokuwa mwanzoni.

"Hapo awali alikuwa na uwezo wa kuihudumia familia yake kwa njia ya kazi zake alikuwa anamsomesha mdogo wake wa mwisho pamoja na kulipa kodi ya nyumba alikuwa akifanya mambo mengi hivyo na swala la kusoma ni jukumu lake pia" alisema

Mbali na hayo msanii Cheni alieleza kuwa Lulu yupo tayari kurudi shule ili aweze kujikwamua kielimu aweze kupambana na maisha hivyo jambo la msingi ni yeye kufikia malengo yake aliyojipangia kwani umri wake bado ni mdogo na ana nafasi kubwa ya kubadilisha maisha yake

Akizungumzia kwa upande wa kazi Dk. Cheni aliweka wazi kuwa endapo Lulu akimuomba amsimamie kazi zake atafanya hivyo kwani yote ni katika nia njema ya kumfikisha msanii huyo katika malengo aliyojipangia.

HONGERA SANA LULU KWA KUFIKIRIA KURUDI SHULE, KIPAJI UNACHO HIVYO KUPITIA ELIMU NA KUJIPANGA UPYA UNAWEZA KUFIKIA MAFANIKIO AMBAYO HUKUWAHI KUYAOTA KUPITIA KAZI ZAKO ZA FILMS. MUNGU AKUONGOZE UFIKE MBALI ZAIDI.(credit:tanzaniaone.com)

                            

No comments:

Post a Comment