Shows za hivi karibuni za mwanamuziki Diamond Platinumz zimeonekana kukosa watu hivyo kuanza kuzua minong'ono kuhusu issue ya mganga aliyeibuka hivi karibuni kudai kumpaaisha mwanamuziki huyo lakini Diamond akikanusha kwa nguvu zote huku mganga huyo akidai Diamond amekiuka maagizo na makubaliano yao.Baadhi ya shows zake za hivi karibuni Zanzibar na Mwanza zimekosa watu,
katika show yake ya Zanzibar 22 January
Bwawani Pemba ilisadikika palikuwa na watu wasiozidi 50 na viti
vingine vyote vilikuwa vitupu. Kiingilio kilikuwa 10,000 kawaida na 15,000
VIP. show yake aliyofanya usiku wa Valentine Jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest pia inasemekana kubuma, Kiingilio kilikuwa 20,000. Hata hivyo baadhi ya watu wakiwemo mashabiki wake wameonekana kumtetea mwanamuziki huyo wakisema ni kawaida kwa wasanii wakati wengine wakidai shows zake huko nyuma huwa zinajaza sana watu. wengine wanasema kuwa amezidi kuimba nyimbo za mapenzi mpaka kukosa mvuto hata siku ya Valentine day na kuendekeza mademu kunamshusha kisanii. Hata hivyo hizi ni fununu tu na dua la kuku........Diamond mwenyewe ndiye anajua ukweli.
Je wewe una lipi la kuongea?
Picha 2 za mwanzo ni za show yake ya Zanzibar na picha ya mwisho chini ni show yake ya Mwanza.
I have selected positive a lot of Useful information out of this source. I’d love to visit it more than and over again.
ReplyDeletehelp with public administration thesis papers