Pages

Thursday, January 31, 2013

WEMA SEPETU APATA SERENGETI BOY MPYA ILI KUMKOMOA DIAMOND

Mrembo asiyeishiwa vituko na anayeongoza kwa kutajwa na vyombo habari Wema Sepetu ameamua kuanzisha mahusiano mapya kwa kile kilichoelezwa kuchoshwa na kujipoza na kulipa kisasi kwa DIAMOND Wema amejikuta akinasa kwa kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Haidary Cavilla ambaye mwanzo jamaa huyo alikuwa ni mchumba wa marcy Galabawa aliyekuwa mshiriki wa miss Tanzania mwaka 2000.
Taarifa zinasema kuwa wema amenasa kwa Haidary kufuatia mkwanja mrefu alionao jamaa kilisema chanzo hicho kiukweli jamaa anamiliki mkwanja mrefu sana japo ni kijana mdogo sana kiumri inawezekana wema kampita kwa miaka mingi sana ila kutokana na pesa alizonazo dogo wema hajaangalia hicho yeye kaangalia pesa kiliendelea kutiririka chanzo hicho. Inasemekana wema alidata kwa kijana huyo ambaye ni serengeti boy wa wema kwa sasa kutokana na mambo mawili kwanza pesa pili kumchanganya ama kulipiza kisasi kwa Diamond ambaye alikuwa mtu wake na ni baada ya kuweka ile picha waliyolala na peny vj japo peny alikanusha na kusema ni movie jambo ambalo halimuingii wema akilini.
Ili kuonyesha jeuri ya pesa jamaa ameamua kumnunulia wema gari aina ya Q7 Aud jambo lililomchanganya wema,chanzo chetu ambacho kipo karibu na wawili hao kimesema Haidary amemnunulia wema gari hiyo iliyozidi bei gari ya diamond aina ya prado ili kumuonyesha diamond kuwa wema ni zaidi yake alisema mnyetishaji huyo. Habari zaidi zinasema kuwa wema na serengeti boy wake huyo wamepiga picha hizi wakiwa nymbani kwa wema sepetu na hatimaye mtu wao wa karibu kuzivujisha mtandaoni jambo lililomkera hidary japo kwa wema ilikuwa furaha kwani anaamini atakuwa amelipa kisasi kwa Diamond.
Kusema kweli kaka mimi nakaa na wema kwa karibu sana nachokuambia wema bado mapenzi yake yapo kwa diamond ila hana jinsi tu,,mimi binafsi nimemuona mara nyingi akiumia sana juu ya kuachana kwake na diamond unajuwa wema ana mapenzi ya kweli na akipenda huwa hajifichi ila ana bahati mbaya aliowapenda wote hawajampenda kwa dhati labda huyu wa sasa tuombe mungu,,maana toka wameachana na diamond hapa katikati wema alikuwa kadata kila akisikia diamond yupo na huyu mara huyu wema alikuwa mtu wa mawazo tu kilisema chanzo chetu
Nadhani utakubaliana na mimi kuwa pamoja na kuwa na mashabiki wengi Wema sepetu ni mrembo ambaye hana ujanja wa kukwepa skendo chafu zinazomkabili kubadilisha wanaume kama nguo Hawa ni baadhi ya wanaume waliowahi kutoka nae au kudaiwa kuwa na wema kimapenzi MR BLUE, T.I .D, MAREHEMU STEVEN KANUMBA, JUMBE YUSUPH, CHAZ BABA, DIAMOND PLUTNUMZ CLEMENT ( Bado wako pamoja) HAIDARY CAVILLA,,ALIYEMNUNULIA Q7, Na wengineo......(credit:thesuperstar)

No comments:

Post a Comment