Pages

Tuesday, January 15, 2013

RAY JITAZAME UPYA KWA AJILI YA HESHIMA BONGO MOVIE

Muigizaji maarufu wa filamu afrika mashariki Vicent Kigosi maarufu kwa jina la Ray anaonekana kutokujua kuwa muonekano wa mtu huweza kupeleka mtazamo/ujumbe flani kwa jamii aidha uwe ujumbe hasi au chanya. Ray muda wote anaonekana kuvaa kipuli tena bila kujali mazingira aliyopo ! kipuli ni sehemu ya pambo la mwili ambalo kama nguo pia huvaliwa kutokana na mazingira na hata wakati lakini kwa Ray ni tofauti maana huvaa mpaka maeneo ambayo hayaruhusu pambo hili kwa mwanaume hasa kwa jamii za kiafrika kama vile msibani au kukutana na wazee wenye heshima au viongozi wa nchi.Nimeamua kumjadili Ray siyo kama mtu binafsi ila muigizaji ambaye ni kioo cha jamii na pia kiongozi(mwenyekiti)wa bongo movie.Hivi karibuni katika msiba wa muigizaji marehemu Sajuki pia muonekano wa Ray haukuwa na mantiki wala maana yoyote zaidi ya kuleta mtazamo hasi kwa jamii kuhusu waigizaji na jamii kwa ujumla. pia...
Wiki iliyopita Ray alikuwa na wasanii wenzake Kondoa mkoani dodoma katika kijiji cha Kwadelo ambapo walienda kuzindua mradi wa kilimo kwanza na kuktana na wazee wenye heshima zao tena wengine wakionekana kuwa ni watu walioshika dini kiasi cha kuomba dua wakiwa na wasanii hao lakini muonekano wa muigizaji huyu pia haukuwa wa kuridhisha tofauti na wasanii wenzake wa kiume kina JB na Single Mtambalike(Richie)maana Ray pia alikuwa amevaa kipuli mbele ya wazee wenye heshima hivi kama alijitambulisha kwa wazee na wanakijiji alijitambulisha kama kiongozi wa wasanii wa bongo movie au? maana mazingira yale na hata shughuli yenyewe waliyoitiwa au kuifuata(kilimo kwanza) haikuhitaji muigizaji huyo kuvaa kipuli....
Hivi karibuni magazeti yaliripoti habari ya Ray na Mayasa kumjia juu muigizaji mwenzao Thea kwa kukiri na kuanika kuwa bongo movie kweli kuna uchafu na mambo ambayo hayapendezi kwa jamii na kina Ray kumjia juu Thea kuwa anawaanika bongo movie kwenye media sasa hapa walikuwa wanataka kuficha nini wakati taswira za viongozi wa Bongo movie zinajionyesha waziwazi!. ukimuangalia sana Ray ni kama vile aligombea nafasi ya uongozi Bongo movie ili afiche uchafu wa club hiyo na siyo kutatua matatizo hii ni kwasababu uvaaji wake yeye kama kiongozi wa bongo movie ni sehemu ya tatizo.Kwa ufupi ni kuwa Ray hataki mambo ya bongo movie yafike kwenye media au anaamini kuwa bongo movie ni safi ila magazeti ya udaku ndiyo tatizo. Baadhi ya watu siku hizi wanakiri kuwa kumtazama Ray kama msanii kunachosha maana anavyoonekana kwenye filamu zake karibia zote ndiyo utamkuta hivyo hivyo mtaani mpaka kwenye matukio ya kijamii na kipuli muda wote. Hivi mbona mastaa wa nje ukiwaona wakiwa kwenye screen ni tofauti na ukiwaona wakifanyiwa interviews kwenye Tv achilia mbali mtaani !. Sina ubaya na Ray bali nimejaribu kufikisha mawazo yangu na kama ni kipuli anaweza kuvaa kutokana na uhusika flani pale inapobidi maana kuna filamu kibao kavaa pambo hili lakini halikuendana na uhusika au scene husika, Na nje ya filamu kuna baadhi ya maeneo anaweza kuvaa lakini si kila sehemu.
photos from:raythegreatest

No comments:

Post a Comment