Wednesday, January 16, 2013

MUIGIZAJI" UKWA" AKIRI KUMZIMIKIA JACKLINE WOLPER

Muigizaji wa Swahiliwood Nicholous Ngoda akiwa katika filamu moja na Ukwa wa Nigeria sijui hiyo filamu itakuwaje maana wote wanaweza kukufanya ucheke. Nicholous Pia anaigiza na msanii mwenzake mwingine wa kibongo anayeitwa Meya Shabani(Aki wa bongo)ambaye pia kwa namna flani anafanana na Aki wa Nollywood.msanii huyu amezaliwa mwaka 1986 wakati sanaa alianza mwaka 2000 wakati akiwa shule ya msingi Ubembe, amehitimu kidato cha nne Mzinga high school mwaka 2009.Anapenda sana kazi za muigizaji wa Swahiliwood Jacob Stephen maarufu kama JB. Nilibahatika kupata nafasi ya kuchonga na msanii huyu hivyo nikaone pia niwaletee mashabiki wake machache about him.Tiririka nayo............
SWP:Filamu yako ya kwanza kuigiza inaitwaje na ulijisikiaje kwa mara ya kwanza ulipoanza kuigiza filamu?
NICHOLOUS:My first film was PASTOR MYAMBA THE(The trial), nilijisikia kama miongoni mwa watu maarufu duniani kwa kukutana na mastaa nilio pangwa nao na pia siku niliyosikia inatoka sikupata usingizi nikiisubiria kwa hamu.
SWP:Ni kitu gani muhimu sana ambacho wewe kama muigizaji unakipenda sana unapokuwa shooting na nini unakichukia?
NICHOLOUS:Napenda kumuona msanii mpya /underground akijifunza kitu toka kwangu Sipendi kumuona mtu akichelewa kuja location kwa uzembe.
SWP:unafikiri ni kweli baadhi ya waigizaji hawana vipaji lakini wanapewa nafasi na waongozji katika filamu za kibongo? na unafikiri sababu ni nini?
NICHOLOUS:Hilo ni kweli 100% sababu ni ukosefu wa ajira kwahiyo watu wanajaribu bahati yao kwenye sanaa.
SWP:Tayari wewe ni mtu maarufu so vipi usumbufu kutoka kwa mademu?
NICHOLOUS:Nashukuru MUNGU body structure yangu inanilinda mademu wengi wanashindwa kunitambua kama ni mkubwa au la.
SWP:Ukipewa nafasi ukutane na star yeyote wa kike Tanzania na star wa kimataifa nani atakuwa chaguo lako?
NICHOLOUS:Tanzania nampenda Jackline Wolper, mtoni nampenda Vivian.
SWP:Ungependa kuwaambia nini mashabiki wako kwa ujumla?
NICHOLOUS:Wakae mkao wa kula kuanzia mwezi huu na february kuna filamu kali nimecheza zinakuja,UNCLE MPOZEMENYA, WAJASILIAMALI, GOD'S KINGDOM na PATASHIKA.

No comments:

Post a Comment