Pages

Thursday, January 31, 2013

MOVIE REVIEW: KIVULI

STAR CAST: Wastara Juma, Slim Omary Mrisho, DIRECTOR: Leah Mwendamseke(Lamata),PRODUCER: Wajey Film's co.
Pius(Slim Omary Mrisho)anahamia katika nyumba mpya, mkewe Nuru(Wastara Juma) anarudi kutoka masomoni nje ya nchi. baada ya muda Nuru(Wastara Juma) anaanza kuona mauzauza katika nyumba hiyo mpya waliyohamia anamueleza mumewe lakini haamini kutokana na muda mwingi kutokuwa nyumbani akidai ni kutokana na kazi kuwa nyingi.Mauzauza yanazidi kila kukicha hivyo wastara kutotaka tena kukaa katika nyumba hiyo peke yake, mumewe anamletea wafanyakazi wawili mmoja wa kike(house girl)na mwingine wa kiume kwa jina la Senjele(mlinzi),anakaa nao baada ya muda flani wanaanza kuyaona mauzauza hayo na kutaka kuondoka.Hatimaye inabainika kuwa mwenye nyumba alimuua ndugu yake miaka kadhaa nyuma na ndiyo chanzo cha mzimu huo kuua watu katika nyumba hiyo.
Baadhi ya matukio hayakuwa na maana yoyote kuyaweka, Wastara kumpelekea Slim Omar chai kitandani akiwa bado kuamka ni ishara ya poor screenplay . Director alikuwa kawaida, lakini ameshindwa kuangalia kazi ya mhariri kwa ukaribu hivyo post production kukosa ushirikiano kati yake na editor. Hata kabla filamu haijaanza unaona tatizo la editing, subtitle ndiyo usiseme hapa ilikuwa ni kazi kweli kweli maana maneno mengine wala siyo ya kiingereza kwa hiyo sijui yalitoka wapi(grammatical error)"dont(don't),cant(can't),maneger(manager),chaged(changed),enterfere(interfere),nothig(nothing),sincethe(since the)youy(your),congorese(congolese),scripty(script)na mengineyo mengi mpaka mtu unabaki kutabasamu tu kwa hiyo huko nchi za nje sijui itakuwaje wakiitazama.Slim Omary alikuwa normal. Director amshukuru sana wastara na yule house girl kwa performance nzuri. mtu wa costume na make-up bado hakufanya kazi ipasavyo, mzimu haukuonekana kama mzimu kuna sehemu unawaka kama binadamu sehemu nyingine ukiwa umechuja sana. Licha ya hayo ni filamu nzuri itafute na kuitazama kama bado hujaiangalia.(sorry, hatukuangalia music/sound kutokana na sababu maalum)

No comments:

Post a Comment