Wednesday, January 30, 2013

LULU KUCHEZA FILAMU MOJA NA AKI NA UKWA WA NIGERIA LICHA YA KUKUMBWA NA MISUKOSUKO

Muigizaji Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anaweza kupata bahati ya kucheza filamu na wasanii maarufu Afrika kutoka Nigeria Aki na Ukwa licha ya kuwa katika misukosuko ya kukabiliwa na kesi ya mauaji bila kukusudia ya msanii mwenzake Steven Kanumba.Wasanii Nicholous Ngoda(Ukwa wa Tz) na Meya Shabani(Aki wa Tz) wana mpango wa kucheza filamu na wasanii wa Nigeria Aki na Ukwa na muigizaji wa kike ambaye amefikiriwa kuwa lead actress katika project ya filamu hiyo ni Lulu.Akizungumza exclusively na swahiliworldplanet Nicholous(Ukwa wa Tz) amesema "Aki na Ukwa tungependa kuipongeza mahakama kwa kumpa dhamana msanii mwenzetu Lulu na hatimaye kuwa nae uraiani". muigizaji huyo machachari aliendelea kusema "tulikuwa tukimsubiri kwa hamu kwani tunataka na yeye awepo kwenye ile project yetu na AKI NA UKWA wa NIGERIA, Yeye atashiriki kama main character "kwa hiyo kuwepo kwake lupango kunge idororesha project yetu, tunamwombea aendelee kuwa na afya njema hadi siku ya wale jamaa watakapo tua nchini tayari kwa kuanza kazi za kimataifa"

No comments:

Post a Comment