Pages

Wednesday, January 30, 2013

LULU BADO TISHIO, NDANI YA FILAMU MOJA NA JACKLINE WOLPER

Actress wa swahiliwood Jackline Wolper anaandaa movie mpya ambayo itawakutanisha yeye na Elizabeth Michael 'Lulu' itakayokamilika hivi karibuni baada ya msanii huyo kutoka gerezani kwa dhamana Wolper alisema amepata faraja baada ya taratibu na sheria kufuatwa na hatimaye Lulu kupata dhamana so anatarajia kufanya naye filamu mpya itakayoanza kurekodiwa baada ya actress huyo kufika kitaani Alisema kuwa anatarajia atafanya vizuri katika filamu hiyo kwani tangu awali alikuwa akifanya vizuri katika tasnia hiyo ya uwigizaji kabla ya kupatwa na matatizo "Nimeshampokea Lulu tangu moyoni mwangu kwani kule alikokuwepo si sehemu nzuri na ukiangalia bado ni mtoto mdogo hivyo inaumiza sana" alisema Wolper
Filamu hiyo ndiyo itakayokuwa ya kwanza kuchezwa na Lulu baada ya kufika Uraiani Wakati huo huo Rose Ndauka alisema ni wakati wa wasanii kumpokea mwenzao kwani wote ni familia moja na wanahitaji kushirikiana katika kila hali Alisema kuwa ukiangalia umri wa msanii huyo ni mdogo hivyo bado ana nafasi kubwa ya kutengeneza maisha yake na kuangalia wapi amekosea na wapi anapaswa kurekebisha Naye actor Single Mtambalike 'Richie' alisema anashukuru kuona sheria imechukua mkondo wake na hatimaye kuachiwa kwa dhamana hivyo kwa upande wao ni faraja kubwa kwani wote ni familia moja Alisema anaamini sasa ataweza kujipanga na kufanya kazi vizuri kwani ana kipaji na bado watanzania wanamuhitaji kulingana na uwezo mkubwa alionao kwenye tasnia hiyo.
credit:bongoclan

No comments:

Post a Comment