Saturday, January 19, 2013

JACKLINE WOLPER AMSAIDIA SHAMSA FORD BLACKBERRY

STAA wa filamu za Bongo, Shamsa Ford ametangaza simu yake ni ‘kimeo’, cha ajabu msanii mwenzake, Jacqueline Wolper akatoa yake aina ya Blackberry na kumkabidhi bila malipo Ishu hiyo ilijiri kwenye arobaini ya mama wa Mtangazaji wa Kipindi cha Take One cha Clouds Tv, Zamaradi Mketema ambapo Shamsa alionesha simu yake ilivyokuwa imechakaa na kufungwa kwa ‘rababendi’. Shamsa aliendelea kuomba msaada huo kwa kila msanii wa kike aliyekuwa anaingia kwenye hitima hiyo ambapo alikuwa akipiga kampeni kwa kusema kuwa ameshindwa kununua simu nyingine kutokana na kukosa fedha kwa sababu ya majukumu kibao aliyonayo kwa sasa.
Muda mfupi akiwa anaendelea na kuinadi ‘shida’ yake hiyo, aliingia Wolper ambapo alikwenda kukaa karibu na Shamsa. Shamsa aliitumia fursa hiyo kumueleza shida yake Wolper naye akatoa simu yake aina ya Blackberry na kumkabidhi mbele ya wasanii wengine. Baada ya kupokea simu hiyo, Shamsa alimshukuru Wolper kutokana na moyo wake wa upendo aliouonesha kwake. Wasanii wengine waliokuwepo walibaki kumshangaa Wolper na kumwambia Shamsa azidi kumshukuru mwanadada huyo kwani kilio chake kimeisha. “Yaani namshukuru sana Wolper kwani amenileta tena kwenye ulimwengu wa Blackberry kwa sababu nilikuwa nimepotea siku nyingi na sikuwa napata habari mpya za mjini,” alisema Shamsa
credit:the superstars

No comments:

Post a Comment