Pages

Friday, January 25, 2013

DIRECTORS NA WAIGIZAJI WA KITANZANIA TUJIFUNZE HAPA

Kwanza ningependa kuwapongeza wadau wote ambao kwa sasa wanaonekana kuwa mstari wa mbele ili sanaa ya filamu nchini ipate kutambulika rasmi na kuwa na manufaa kwa wasanii hasa kiuchumi.katika kundi la wapiganaji hawa wapo film directors au waongozaji wa filamu ambao wamekuwa wakijitahidi licha ya kwamba baadhi yao kazi zao bado haziridhishi licha ya kuwa na miaka kadhaa lakini films wanazoongoza zinaonekana kuwa na makosa yale yale au kukosa ubunifu. Leo nisingependa kwenda mbali zaidi ila ningependa kuligusia suala la utafiti katika filamu kabla ya ku-shoot.Takribani kama wiki 2 sasa nimeangalia filamu 5 za kitanzania lakini 3 kati ya hizo haziridhishi hasa katika uongozaji wake 2 zikiwa zinatia moyo kutokana na tasnia yetu ilipo kwa sasa. Tatizo nililoliona katika films zetu ni kutofanya utafiti hata kidogo tu kuhusu character husika matokeo yake filamu inakosa mvuto wa kukushawishi kuitazama. Niseme tu kuwa katika films kila character ni lazima ifanyiwe utafiti hata kama ni simple kiasi gani, hii ni kwa kuwa katika jamii watu wanaweza kuwa na tabia ya character unayotaka kuionyesha au kucheza katika filamu lakini tabia hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu au jamii na jamii hivyo ni lazima ufanye utafiti kwa kuwa hadhira ya filamu huwa kubwa.Ma-director wakubwa hata hollywood au India kitu kidogo tu hukifanyia utafiti ili wasije kukosa heshima katika kazi zao. madirector wengi wa kitanzania bila hata kujaribu wanafikiri utafiti ni gharama au unahitaji pesa sana na hata muda mwingi kumbe sivyo. hapa nitakupa njia chache tu na rahisi ili ufanye utafiti bila hata kuvuruga muda au ratiba kabla ya kuanza ku-shoot na bila kutumia gharama zozote unazoita kubwa.
1:kwanza, director na muigizaji kabla hamjaanza kushoot weka ratiba hata ya siku moja au mbili utembelee eneo au watu unaofikiri wanaendana na character ya filamu husika au wana tabia sawa na huo uhusika. mfano kama msanii anatakiwa acheze kama polisi au changudoa jaribu kutembea nae eneo la watu hao yaani vituo vya polisi au kwenye madanguro na maeneo ya machangudoa au mpe hata siku moja akawaone ili asome tabia zao tofauti tofauti. Mfano tabia za machangudoa katika filamu za kitanzania karibia zote zinafanana lakini katika hali halisi machangudoa hutofautiana tabia zao na hata namna wanavyojiuza. Nani aliyekuambia kuwa changudoa siku hizi ni kuvaa nguo fupi na kuvuta sigara pekee?. tatizo ni ukosefu wa utafiti
2:pili,Angalia filamu au documentary ambazo unafikiri zinaendana na unachotaka kukifanya. hapa muigizaji na director ni lazima afanye hivi. sijataja usome vitabu au majarida ambayo yanaelezea au yanahusika na character inayotakiwa kuchezwa kwa kuwa kusoma kitabu huchukua muda tofauti na kuangalia filamu. ukiangalia filamu au waigizaji/directors wenzako wamefanya nini kabla yako unapata mawazo tofauti ingawa hapa sikushawishi ufanye copy and paste bali ujifunze na kuchanganya na mawazo yako. waigizaji kibao wakubwa hollywood/bollywood hupewa vitabu wasome kabla ya kuanza ku-shoot. pia hupewa films au documentaries na director husika ili aangalie ajifunze zaidi kabla ya kazi kuanza.
3:Mfuate na kumuomba mtu ambaye ana tabia au hali flani ambayo unataka kuionyesha kupitia filamu yako kama unahisi sehemu husika ya kuiongoza katika filamu husika itakupa shida na kushindwa kuifanya kama unavyota/inavyotakiwa.Aliyekuambia film director anajua kila kitu ni nani?. hiki ni kitu ambacho kinakubalika kitaalam director kumchukua mtu ambaye ana hali au tabia husika ili amsaidie na haijalishi huyo mtu ni nani, huyo mtu pia anaweza kuwa hiyo tabia alikuwa nayo lakini ameacha au hanayo tena. mfano director anaweza kumchukua jamaa aliyewahi kuathirika na madawa ya kulevya au bubu au kiziwi ili amsaidie katika kuwaelekeza waigizaji/muigizaji ili wauvae uhusika ipasavyo. Mfano unaijua filamu ya bollywood inayoitwa Black(2005)hii filamu iliongozwa na veteran director mwenye heshima kubwa sana mpaka hollywood Sanjay leela Bhansal. Hii filmu ilipata high critical scores mpaka hollywood,pia ilipata tuzo kibao mwaka huo kama best film, best director, best actress na best actor na jarida maarufu la la ulaya (Times magazine) likaitaja kama filamu 10 bora duniani kote kwa mwaka 2005 na moja ya films za kihindi ambazo ni lazima uitizame. lakini director wa filamu hii alisaidiwa na kijana mdogo ambaye ni kiziwi na bubu katika kumchezesha muigizaji mkuu kama kiziwi na bubu( Rani Mukerjee)na Amita bachchan nae akiwa katika uhusika mgumu sana katika hii filamu.kama wewe ni director na hujaingalia filamu hii nakushauri itafute uingalie utajifunza sana. jinsi ulivyo muona Rani mukerjee(Tina) katika "kuch kuch hota hai" na utakavyomuona katika Black huwezi ukaamini hata kidogo kama ni yeye kwani hata yeye mwanzoni alikataa kuicheza filamu akisema uhusika ni mgumu hataweza kuvaa lakini director akamwambia I bielieve in you, alipewa muda wa kutosha ili ajifunze alama za viziwi na mabubu.
njia hizo hapo juu ni njia rahisi sana kuzifanya bila kupoteza muda wala pesa ili wasanii wauvae uhusika inavyotakiwa tofauti na wenzetu ambao husafirishwa hata nchi za nje ili kujifunza kabla ya kuanza ku-shoot. Ahsante

2 comments:

  1. Asante sana kwa muongozo wako,nimeipenda sana,tatizo tulilonalo wengi wetu ni kukurupuka ili mradi mtu anastori anataka lazima ashoot hata kama bajeti hairuhusu sembuse mtu kutumia muda wa ziada kuanza kufanya tafiti za wahusika? kweli yatupasa tubadilike,tafadhali endelea na darasa kutokana na tafiti zako pia,nitakutumia kazi zangu nipatapo wasaa ili unikosoe nijifunze zaidi toka kwako! rubuyemajaliwa@yahoo.com

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante sana kwa kupenda nilichoandika na pale inapobidi lazima nitachambua au kuandika kuhusu kasoro na hata kupongeza kuhusu films zetu. thanx again

      Delete