Monday, January 21, 2013

BABY MADAHA: SHILOLE ANATEMBEA NA WATOTO WADOGO

KUTOKANA na bifu linalofukuta kama moto wa kifuu kati ya waigizaji, Flora Mvungi na Zuwena Mohamed ‘Shilole’, staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ ameibuka na kumchana Shilole kuwa analitamani Gereza la Segerea. Akiongea namwandishi wetu, Baby Madaha aliyelinunua sakata hilo, alimtaka Shilole kuacha kumfuatafuata shosti wake (Flora) kwani yeye hana lolote zaidi ya kuropoka maneno machafu. “Eti Shilole anatangaza kuwa atanipiga mimi hebu ajaribu kama yeye mwanamke kweli, mimi haniwezi kamwe. Kwanza hajielewi hata thamani yake, kutwa kutembea na watoto wadogo halafu anajiona staa,” alisema Baby Madaha. Aliongeza kuwa anamshangaa shilole ambaye badala ya kufanya yake kila siku amekalia kuongelea mambo ya flora na mpenzi wake H baba ,Nashangaa mwanamke mzima kukaa kuongelea mapenzi ya watu au ulikuwa unamtaka huyo mwanaume ..alihoji baby madaha ambaye alionyesha kukerwa na kitendo hicho.CREDIT:the superstars

No comments:

Post a Comment