Wednesday, December 26, 2012

WEMA SEPETU, MARTIN KADINDA AND SUPERSTAR

Ni miezi kadhaa sasa imepita tangu filamu ya "Superstar" iliyoandaliwa na kuigizwa na muigizaji maarufu wa swahiliwood Wema Sepetu na waigizaji wengine maarufu kuzinduliwa kwa namna ya aina yake kwa kumleta muigizaji maarufu barani afrika Omotola Jalade kutoka Nollywood na uzinduzi wake kufanyika katika hotel maarufu ya Hyatt Regency. Lakini mpaka sasa filamu hiyo nimejaribu kuitafuta kwa wauzaji ili niitazame lakini sijaiona sijui kama bado haijatoka au la!, ingawa nimesoma kwenye gazeti moja la kila mwezi likimnukuu meneja wa Wema akisema kuwa wasambazaji wanaleta ubabaishaji kwa kutaka kutoa pesa kidogo ili waisambaze tofauti na gharama zake kubwa zilizotumika kuitengeneza mpaka kuzinduliwa kwake na kusemekena zaidi ya milioni 60 kutumika.Hapa nilishangaa kidogo kutokana na maelezo ya Martin Kadinda kama kweli walifanya utafiti kabla ya kutengeneza filamu ya gharama kubwa kiasi hicho na uzinduzi wa gharama tena watu wakiingia bure kwa mwaliko maalum na siyo kwa pesa bila kujua au kuwa na uhakika na usambazaji wake,katika soko la usambazaji wa filamu Tanzania lililojawa na ubabaishaji na unyonyaji kwa wasanii na watengeneza filamu na kukosa sapoti ya kutosha kutoka serikalini, binafsi niliingiwa na mashaka na usambazaji wa filamu hii hata kabla haijazinduliwa kutokana na kutengenezwa kwa gharama kubwa. endelea kusoma.........
-Lakini ukiangalia sana ni kuwa Wema ana uwezo wa kusambaza filamu yake hii na hata zijazo kama uzinduzi ule ungekwenda sambamba na uzinduzi wa kampuni yake ya kusambaza kazi zake maana uwezo anao na siyo kuwa na kampuni ya kutengeneza filamu pekee! mfano kama wema ametumia milioni 60 mpaka filamu kukamilika atashindwaje kununua magari ya kawaida kama vile Nouh hata 2 au 3 ya kuanzia kila moja kwa gharama ya milion 15 kwa ajili ya kusambaza kazi zake nchi nzima na baadaye nchi jirani na kadri anavyozidi kukua kusonga mbele zaidi?.Vile vile Wema ni mmoja wa wasanii ambao wanajitoa sana kuisaidia jamii na hata wasanii wenzake hasa pale wanapopatwa na matatizo kama vile kuumwa kwa hiyo siyo kila mtu anaweza akamsaidia ingawa kumsaidia mwenye matatizo huleta heshima zaidi kwa jamii na mungu kukuzidishia zaidi lakini anatakiwa kuangalia wa kumsaidia na siyo kila mtu ili angalie maendeleo yake kama kuwa na kampuni yake ya usambazaji ili apige hatua zaidi na siyo kutegemea wasambazaji waliopo sasa maana hawajali mtengeneza filamu kupata hasara hata kama mauzo yapo ya kueleweka....
-Jingine ni kuhusu Martin kuwa meneja wa Wema anatakiwa kuangalia hali halisi ya soko la filamu lilivyo Tanzania na siyo kum-manage Wema kama vile wasanii wa hollywood maana hali hairuhusu hivyo na kama hili angeliangalia mapema filamu ile isingetengenezwa kwa gharama kubwa kiasi kile maana matokeo yake ni ubabaishaji katika usambazaji wake hivyo Martin kujuana na watu wengi pekee haitoshi kuwa meneja bali anatakiwa azichange vyema karata zake kwa kufikiri kwa undani zaidi hali ilivyo katika usambazaji....
Mwisho, filamu ile kama ingetoka muda ule ule nafikiri ingeuza vizuri tu kurudisha gharama na faida ya kutosha pia maana ilitangazwa sana na kupata promo ya kutosha hata kwenye media kutokana na vituko visivyoisha vya Wema na ujio wa Omotola ulichochea zaidi ijulikane, lakini kama bado haijatoka na ikitoka sasa mauzo yake yanaweza yasifikie kama ingeuza wiki moja au mbili baada ya kuzinduliwa maana wengi tayari wanaonekana kuisahau hivyo kama haijatoka bado basi ni vizuri ikapigiwa promo tena na kama wahusika wasipokuwa makini usishangae ikatua kwenye mikono ya maharamia na kuanza kusambazwa kwa bei cheee...

No comments:

Post a Comment