Pages

Tuesday, June 4, 2013

WALTER DE NGONDE KUFANYA KWELI NA RJ COMPANY NA IRENE UWOYA.

Models wengi  kwasasa wanaingia kwenye tasnia ya filamu Swahiliwood ili kuonyesha vipaji vyao vya kuigiza pia. Mastaa wengine wa Hollywood pia walianza kuwika kwenye mitindo kabla ya kutia team kwenye uigizaji. Baada ya models wa Tanzania kama vile Lota Mollel na Em Evans kuingia kwenye movies, model mwingine alieamua kuingia kwenye tasnia ya filamu ili aonyeshe makali yake ni Walter de Ngonde. Walter tayari ameshacheza katika filamu ya Poor Minds ya Yusuph Mlela ambayo ipo sokoni tayari na pia amecheza kwenye filamu nyingne na mastaa wengine wakubwa kama vile Cloud katika filamu ya Shahada, Wrong Ideas kutoka Rj Company na The Process kutoka 5 Effects ambayo Irene Uwoya pia ni mmoja wa mastaa wa hiyo filamu ingawa amecheza supporting roles zote but we want to see him as a hero in movies.

 Kwa upande wa mitindo kwasasa amejikita zaidi katika matangazo na sio runaway shows. Pia tayari ana uzoefu mbele ya kamera licha ya kuwa upcoming actor kwakuwa alikuwa mshiriki wa Dume Challenge na kufanikiwa kufikia episode ya 8 kati ya 12. Pia aliitwa katika usaili wa shindano la Big Brother Africa 2013 ingawa bahati haikuwa yake ya kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa Tanzania katika mashindano hayo. Walter anapenda kazi za Yobnesh Yusuph(Batuli), Irene Uwoya, Stanley Msungu na Slim Omar. Ndoto zake ni kufanya kweli kwenye tasnia ya filamu hivyo kaeni chonjo. Look photos of the sexy actor below.............


1 comment:

  1. This is good news....u will definitely make it ma man.......keep on the hard work.....!!!!...

    ReplyDelete