Pages

Friday, May 24, 2013

BATULI AFUNGUKA KUHUSU BABA WA MTOTO WAKE KUDAIWA KUWA NI RAY.

Siku za hivi karibuni kumeibuka madai kuwa actress Yobnesh Yusuph(Batuli) amezaa na muigizaji mwenzake Vicent Kigosi(Ray) kwa mtoto wa Batuli anayeitwa Jaheim kudaiwa kufanana sana na Ray na hata baada ya Batuli kuweka picha za mtoto huyo facebook baadhi ya watu walitoa maoni na kuuliza mbona mtoto amefanana sana na Ray na Batuli kutotaka maswali hayo akionyesha kuchukizwa na kauli kuwa amezaa na Ray. Wiki takribani mbili wasomaji wa Swahiliworldplanet walituma ujumbe kutaka jibu kama Batuli amezaa na Ray au la!.

Swahiliworldplanet kama kawaida yake ilimtafuta Batuli na kumueleza kila kitu ukiwemo ujumbe wa mashabiki wake na muigizaji huyo kusema kuwa ni kweli mwanae amefanana sana na Ray na suala hilo pia linaleta mvutano hata kwa wasanii wenzake lakini amesema kuwa hayuko tayari kuliweka wazi suala hilo kwa sasa ila atalizungumzia kwa kina siku zijazo ili watu na mashabiki wake waelewe kila kitu. "Ni kweli mwanangu amefanana sana na Ray hili linaleta mvutano hata kwa wasanii wenzangu. Ipo siku nitalijibu swali hili kwa ufasaha zaidi ila kwa sasa sipo tayari kuongea chochote" alisema muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto wa aina yake. Mtoto huyo pia anadaiwa kuwa na kipaji cha uigizaji na anatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza hivi karibuni katika filamu inayoandaliwa na Batuli mwenyewe. Angalia picha ya Batuli na mtoto wake hapo chini......................

                                           Batuli katika pozi
Batuli akiwa na mwanae Jaheim anayedaiwa kufanana sana na Ray

6 comments:

  1. Bado hatujatosheka muhoji ray hawa wanatuficha ukweli pale leaders ukiwauliza wasanii wanasema kweli ni wa ray iweje leo watufiche?

    ReplyDelete
  2. MDAU NIMEPENDA COMMENT YAKO WANATUFICHA NINI WAKATI UKWELI UPO WAZI? RAY NA BATULI MTOTO MI JAMBO LA BARAKA SISI NDIO MASHABIKI WENU TUNA HAKI YA KUJUA HILI HAIWEZEKANI MITANDAO IANDIKE HABARI HII HALAFU KILA WAKATI CHA MSINGI NI KUWEKA BAYANA KUNA NINI KATI YENU? KILA MMOJA HAYUPO TAYARI KUSEMA CHOCHOTE WHY? SWAHILIWORLDPLANET TUNAOMBA UWAHOJI TUSIKIE SAUTI ZAO HALAFU SISI TUTAJUA KUPITIA SAUTI ZAO NANI MKWELI NA NANI MUONGO. FLORA

    ReplyDelete
  3. I really hate it. Ukweli umuweka mti huru Ray acha upuuzi mwanamke huwa hana ujasiri ila wanaume ni viongozi tamka tujue kama una mbegu au huna. Ujinga wa kutokuwa tayari hatuutaki tell us the truth.

    ReplyDelete
  4. Nilikuwa nahisi ni uvumi tu, now I realize hawa ni baba na mama. Congratulation Ray umezaa na mwanamke mrembo sana. Batuli hongera pia.

    ReplyDelete
  5. Kitanda hakizai haramu.

    ReplyDelete
  6. Mtoto ni wa Ray sie tunaujua ukweli tunashangaa wanakataa nini

    ReplyDelete